Wazazi Wanaweza Kuwa Kikwazo cha Ndoa Yenu - EDUSPORTSTZ

Latest

Wazazi Wanaweza Kuwa Kikwazo cha Ndoa Yenu


 NIANZE na neno kidogo; uhusiano sahihi ni ule ambao una manufaa ya baadaye. Nikusihi rafiki, hakikisha unaishi na mtu ambaye unaamini ni sahihi na si kutazama maslahi. Usikubali kuishi katika penzi ambalo halina muelekeo. Ni lazima kila wakati ulitathimini penzi lako na kuona kama lina uhai mrefu au ni la muda mfupi.

Kama huoni ‘future’ ni vyema kujiengua. Ni vyema kusitisha safari ndefu ambayo haitakuwa na tija siku za usoni. Kupanga ni kuchagua, chagua kile unachoona kitakuwa ni sahihi kwa manufaa ya baadaye. Kumuacha umpendaye inauma lakini inapobidi muache ili usije  kuumia mara mbili baadaye atakapokuacha solemba.

Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Turudi sasa katika mada yetu ya leo kama inavyojieleza hapo juu. Kwa hakika hakuna ubishi kwamba wazazi wana mchango mkubwa sana kwa watoto katika suala zima la mahusiano. Wazazi wametangulia kuliona jua. Wamekutana na changamoto nyingi za maisha. Wana uzoefu wa kutosha katika maisha na uhusiano kwa ujumla.

Lakini kwa upande mwingine, wazazi haohao tunashuhudia wakisababisha tafrani kwa wapendanao. Wanazuia ndoa. Wanawapangia vijana wao watu wa kuwa nao na mambo mengine mengi.

Inapotokea mvutano wa wazazi katika suala la ndoa, tatizo linawakumba vijana husika. Wanayumbishwa na mwisho wa siku wanakosa kitu cha kufanya. Watakubali kuoana halafu mmoja wao atengwe au ndoa ivunjike.


Wataathirika kwa sababu wao wanaweza kuwa wamekubaliana kwa hali yoyote lakini wazazi wa upande mmoja kwa sababu wanazozijua wao, wanaweka pingamizi na ndoa inasuasua kuanzia hapo. Tujifunze kidogo kupitia mfano huu;

“Anko naomba ushauri, nimeishi katika uhusiano na mwenzangu kwa takribani miaka mitano sasa. Kiukweli yeye ananipenda na mimi nampenda sana. Tulipanga kufunga ndoa mwaka jana lakini ndoto hiyo haikuweza kutimia kutokana na msukumo wa wazazi wangu. “Yeye ni dini tofauti na mimi, wazazi wangu wamebobea kwenye dini na hata mimi pia. Wamenizuia kabisa nisibadili dini, wanasema nikithubutu tu wananitenga.

“Wakati huohuo mwenzangu naye wazazi wake nao wamemzuia. Kinachoniuma zaidi ni kwamba sisi wenyewe hatuna tatizo, tumekubaliana kufunga ndoa hata bomani kila mmoja abaki na dini yake lakini wazazi wangu hawataki hata kusikia suala hilo, tafadhali nishauri nifanyeje ili kunusuru ndoa yangu?”
TUJIFUNZE SASA
Kupitia mfano huo tunaona ni jinsi gani nguvu ya wazazi inavyoweza kupenya kwa vijana wao hadi kufikia hatua ya kukwamisha suala la ndoa.

Kwanza, wazazi wanapaswa kusikilizwa lakini katika suala hili ni vyema wakakupa mwongozo mapema, wasisubiri wakati mambo yamefika mbali. Tangu awali, wakueleze nini unapaswa kufanya katika kuelekea kumpata mwenza sahihi. Awe na vigezo gani? Mwenye hofu ya Mungu? Mwenye rekodi za aina gani?

Zaidi ya yote inapotokea mgongano tayari mmeshafika mbali, omba busara za viongozi wa dini, watu wazima walio pande zote mbili na mtapata muafaka. Msifanye haraka, kuweni na msimamo wenu lakini zaidi ombeni busara za watu wazima, nakuhakikishia mkifanya jambo hilo kwa imani, hata kama mtachelewa lakini mtafanikiwa.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz