Akina Dada, Sio Kila Ex Wako Anayeomba Mrudiane Anamaanisha. - EDUSPORTSTZ

Latest

Akina Dada, Sio Kila Ex Wako Anayeomba Mrudiane Anamaanisha.


 Sio Kila EX wako anayeomba Mrudiane anamaanisha! Wengine huomba kurudi ili wakutesti tu jinsi ulivyo Mbulula,jinsi usivyo na msimamo na jinsi ulivyo CHEAP na huna Misimamo wala Future.

Jitu mmeachana miezi 6,leo linakutesti lirudishe majeshi,na wewe ulivyo kiazi,upo-upo tu,ina maana miezi yote hii ulikuwa umeganda unasubiria rehema zake ama??

Kurudia Matapishi ya EX ukitegemea Amebadilika ni Sawa na Kupika Sufuria la Makande kwa Mshumaa,Utaambulia Masizi tu..
Kipi kipya kakiona kwako hadi arudi??Nini Kilimshinda huko nyuma ambacho leo anakiweza anataka kurudi??Akafie Mbele huko.

Pakua App ya 'EDUSPOTSTZ (LITE VERSION)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

KUWA NA MSIMAMO,Ukisema Its Over umaanishe,sio unakuwa na hisia zinapepea tu kama Bendera ya Katibu Kata wa Kishumundu…Mtu kama Hajielewi achana nae,siku akijirudisha mwambie kwanza akapimwe Minyoo ya Kinyarwanda.

Umekazana kuwaambia marafiki zako ‘Siku hizi hakuna Mapenzi ya dhati watu wote Majanga tu’,nani amekwambia hayapo??Yapo sana ila wewe unatumia mbinu tofauti..Huwezi kusoma Degree ya Law halafu u-apply kazi ya Chief Accountant wa Bodi ya Tumbaku…Kila siku utasingizia Balance Sheet haina Jurisprudence..Lawyers mmenielewa!

Acha kudate watu wasiojielewa,Usidate kwa sababu uko lonely,Usiwe desperate kuingia Mahusiano kwa sababu shosti zako wanakusimulia walivyopelekwa Ruwenzori Waterfalls..Ingia kwenye Mahusiano pale Moyo wako ukiwa tayari na mtu uliyemfia kihisia na amekuwa approved na Veins,Auricles,na Aorta za Moyo wako kwamba He/She is really the One..

Unadate na mtu ambaye mustakabali wake mwenyewe haujui,ukimuuliza anataka kuwa wapi ndani ya miaka 5 ijayo anakwambia Mungu anajua dont worry,halafu BBM na Instagram unajiita Baby Ake Mie Iam in Love..Utaishia kufua boxer hadi kucha zinukie gololi!

Mbwa kamwe hashughuliki na kesi za Paka kufungiwa kabatini.Date the Right Person,With Right reasons,in a Right Time uone kama Mapenzi hayapo.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz