Kabla Hujalalamika Mkeo Ana Tabia Mbaya Jiulize Mara Ya Kwanza Unampenda Mlikutana Wap? - EDUSPORTSTZ

Latest

Kabla Hujalalamika Mkeo Ana Tabia Mbaya Jiulize Mara Ya Kwanza Unampenda Mlikutana Wap?


Mpenzi wangu malaya,mlevi,anatumia hela vibaya,ana mashoga sana,hanisikii mpenzi wake na mengine mengi hizo ni moja ya kauli watoazo wapenzi wakiwatuhumu wenza wao.

Ila nadhani katika kitu ambacho watu hawazingatii ni kwamba sehemu ya kwanza uliyokutana na mpenzi wako ukampenda ndio sehemu hiyo hiyo itakupa uhalisia wa tabia za mpenzi ambaye umempenda.

Wakati mwingine watu wanaamini naweza mkuta mazingira flani na nikambadilisha akawa mke/mume bora na wakasahau hiyo ni sawa na kamari kuna kula na kuliwa.


Hakuna kitu ambacho mtu unatakiwa kuzingatia kama sehemu ya kwanza jicho lako lilipotazama na kumuona huyo unayemuita mpenzi.

Umemkuta mtu bar,kijiweni,kwenye vigodoro,kwenye danguro,na sehemu zingine za ajabu halafu unaanza kulilia mpenzi wako ana tabia mbaya ukasahau mazingira yalishamuathiri kabla ya wewe kumuona.


Ndio mana mkiristo sana atatafuta mke mwenye dini kanisani,muislam sana atafafuta mwanamke/mume anayejistiri na kwenye mazingira ya heshima,mchapakazi atapatia mpenzi kazini.

SASA NA WEWE LEO JIULIZE JE MPENZI WAKO MLIONANA WAPI MARA YA KWANZA NDIO UANZE KULALAMIKIA TABIA ZAKE.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz