;
UTAMU WA MAPENZI 01 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 27 June 2020

UTAMU WA MAPENZI 01

UTAMU WA MAPENZI 01

BINADAMU bwaana hata ukiogelea watakwambia unawatimulia vumbi, paaaambeee shoga! We endelea kunishangaa Anti Naa badala ushangae mlango mkubwa unalindwa kwa kufuli dogo, heee heeeeiyaaaa!  Shoga umbeya huu unaweza kujikuta unakata kiu kwa mate na kudhani umekunywa maji! Mji mzito huu wangu na kama ujuavyo mambo hayaishi, kutwa Anti Naa naletewa malalamiko kwenye ndoa na wengine hawajaoa, jamani mnitue basi wakati mwingine!

Ni heri ucheke na jirani anayevaa dera ipo siku utamualika kwenye 40 ya mwanao kuliko kucheka na anayevaa jinzi ipo siku atakwapua mumeo, upo nyonyo? Wanakwambia kahaba naye ana ‘future’ ndiyo maana hapunguzi bei, wareeee reeeee!

La leo shoga bora la jana! Ukisubiri urithi wa viatu mwisho wa siku utatembea peku mjini! Hivi kwa nini kila siku mnataka niongee na nyinyi kitu kilekile? Kwa sababu mnajua nawafunda basi mnakosea makusudi ili mfundwe? Sikilizeni niwaambie, siku zote kichaa hajipeleki hospitali na ukiona unakosea ujue mi siyo daktari wa kukufanya ukosee, shuuutuuuuu!

Nimekwazika nikasema lazima nilitoe maana liliniganda kwenye koo halitoki kwa maji, juisi wala bia! Umekubali mwenyewe kuishi na mumeo, amekuudhi kidogo basi unahamishia makosa yake hadi kwenye sita kwa sita, domo umerefusha kama gogo la kukatia nyama buchani, fyaaaatuuuu!

Ifike mahali wanawake sisi tubadilike shoga, umeingia katika uhusiano, umekubali kuishi kwa shida na raha, hilo la kukasirikiana linahusu vipi kwenye vitu vya kupeana raha?

Juzi nimetumiwa meseji na msomaji wa kiume akilalamika sana vitendo anavyofanyiwa na mkewe. Ananiambia anakaribia mwezi wa pili sasa hajawahi kupata tunda kwa mkewe kisa alipata taarifa ambazo hazina ukweli kuwa anatoka na jirani.

Aliniambia amejitahidi kujitutumua na masapraizi kibao lakini ni kama anavunja nazi kwa kutumia vidole, mwanamke hasikii, anaweza kuongea naye vizuri lakini ukifika muda wa chakula cha usiku basi atajigeuza mgongo kama gari lililojaa abiria, shuuutuuuuu!

Nikugeukie basi na wewe mwanamke mwenzangu, hivi unajua tunda halina ugomvi na utamu wa chai sukari wala siyo rangi yake au viungo! Mmekosana nyie kwa nini mshirikishe hadi viungo vingine visivyo na hatia?

Na wewe mwanaume, kufa kwa kiu baharini ni kama uzembe wako! Kama mmeku-baliana kuishi pamoja kwenye shida na raha, kwenye hali yoyote iweje chai yako na huyo mwanamke anajua kabisa ili iwe tamu lazima iambatane na sukari kwa nini anakufanyia hivyo?

Kaeni chini na mueleweshane, kama anaweza kukuandalia mapishi ya aina zote, anaweza kukutayarishia hadi maji na kukuhudumia vyote, atashindwaje kukuachia hiyo sukari ukanywa na chai vizuri!

Kwa leo sitaki niongee sana, nyie wote mnaofanyiana michezo kama hii ifike mahali iwe mwisho. Kwanza ni aibu kubwa na kuwapa mwanya majirani kuwasema na pengine kuingilia uhusiano unasikia mara kachepuka na fulani kumbe mchawi wewe.


Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB