Wanawake wengi Duniani wamekuwa wakiangaika huku na kule, ili mradi waweze kupata utulivu katika ndoa ua mahusiano yao, hii inatokana na hulka ya wanaume wengi kuwa na tamaa hali inayopelekea kupungua kwa upendo.
Baada ya kupokea maombi mengi hasa ya kina mama wakilalamika kuhusu ndoa zao kupumulia Oksijeni, Dokta MAJI YA TANGA ameweza kutumia muda wake mchache kuelezea japo kwa ufupi namna dawa hii inavyotengenezwa.
“Inatakiwa wapatikane njiwa wa jinsia mbili yaani Dume na Jike, kisha wapasuliwe na kutolea mioyo yao, kishwa wachemshwe kwenye mafuta ya mti mmoja unaopatikana porini, sitautaja huu mti kutokana na sababu maalum, kisha husagwa hadi kuwa unga unga“.
“Baada ya hapo utachukua njugu mawe nyeusi moja, utachanganya na mti unaitwa ‘Mlama’ pamoja na miti mingine mitatu ya porini, kisha utaisaga pamoja na ile mizoga ya njiwa”, alisema MAJI YA TANGA
Aliongeza kuwa, “endapo mchanganyiko huo akawekewa mwanaume katika chakula, basi mwanaume huyo atakuwa hasemi chochote, mwanamke atakuwa ndio baba na mama yake, kamwe hawezi kuwa na jeuri mbele ya mkewe”.
Pia ametoa angalizo kwa wale wenye nia ya kutaka kuwakomoa na mwisho kabisa kama wewe sio mtaalam wa masuala ya tiba za jadi, basi usijaribu kutengeneza hii dawa maana inaweza ikakutokea puani
