Hivi kuna wakati ulishatamani upate mtu uongee naye akusikilize halafu ulie wee uchungu ukutoke? - EDUSPORTSTZ

Latest

Hivi kuna wakati ulishatamani upate mtu uongee naye akusikilize halafu ulie wee uchungu ukutoke?


Wakati mwingine tunakuwa hatuhitaji fedha chakula ama mavazi.. tunahitaji watu wa kutusikiliza tu.. tueleze hisia zetu vile tunavyojisikia kuonewa kuteswa na magonjwa kunyanyaswa kusemwa vibaya na hata kudhulumiwa na kudharauliwa na wale tuliojitoa kuwapenda kwa moyo wote....
Ni sahihi kabisa kufanya hivi ili kukusaidia kuuondoa uchungu moyoni lakini naomba nikushauri leo....
Unapojisikia mpweke mwenye huzuni unayetamani kulipa kisasi hasira na uchungu vimekujaa hebu mfungukie Mungu .. Mweleze unavyojisikia..I
Mungu anatarajia tumpe nafasi ya kwanza tunapolemewa ili atusaidie... Anasema...
Njooni kwangu ninyi nyote mnaosumbuka na kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha...
Pia akasema "Duniani mnayo dhiki lakini jipeni moyo mimi nimeushinda Ulimwengu"
Inuka Semezana Naye..Na Mungu akutie Nguvu Katika Siku Yako leo.
Pale unapoona umechoka na kukata tamaa,kuishiwa pumzi na mbinu ndipo Mungu huanza kuchukua nafasi ya kukutetea......🙏🏽🙏🏽🍒
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz