USIHUKUMU HISIA ZA MTU KWA KUTUMIA HISIA ZAKO! - EDUSPORTSTZ

Latest

USIHUKUMU HISIA ZA MTU KWA KUTUMIA HISIA ZAKO!


kuna mdada alikutana na mkaka wakati wako safarini... yule kaka akamuomba mdada namba ya simu. njian akamnunulia kila kitu alichotaka, alipofka stand mkaka akamlipia usafiri mpka nyumbani kwao
bas wakawa wanawasiliana kila siku. siku nyingne anamuita wanatoka wanakula na kunywa na hela anampa.
yule dada akawaambia marafiki zake kua nimepata bonge la bwana jamani nitake nini mimi nisipewe??? mashoga wakamwambia weeee hebu mjaribu tuone.
yule dada akampigia yule jamaa akamwambia leo nipo nipo tu natamani kutoka ila sina hela ya saloon nimemiss sana kwenda club na marafiki zangu. yule jamaa akamwambia ok.
baada ya kukata simu akamtumia lak 3 ya saloon na kumwambia kama isipimtosha aseme kwa njia ya sms.
Wenzie wakasema loh!, shoga bwana umempata.
ilipofika jion yula mwanaume akapiga simu kwa yule bintu akamuuliza club gani mnakwenda???
yule dada akataja club wanayotaka kwenda. Yule bwana akamwabia basi namtuma mtu aje awachukue mie mtanikuta huko
baada ya muda yule dada akaenda yeye na jopo lake, walipofika wakanywa, wakala na kucheza. wakarudishwa nyumbani kama walivyoahidiwa.
siku ya pil yule bwana akamwambia yule dada nataka kuzungumza na wewe ila tafadhali naomba uje peke yako. yule dada akajiandaa akaenda walipopanga wakutane.
Alipofika na kukutana mvulana huyo. na maongezi yao yakaanza bila kuchelewa.
Yule kaka akamwambia nimetoke kumpenda sana rafiki yako yule mweupe mweupe naomba ukamwambie hisia zangu hizi wala sina nia ya kumchezea. nitamuoa kabisa.
yule dada kwa mshangao, akamwambia mimi je??? yule kaka akamuuliza wewe nini??
yule dada akamjibu mimi utanipeleka wapi sasa jamani... kwa hiyo mimi ndio unaniacha? kosa langu nini jamani mpenzi?
yule kaka akamwambia mimi sikuwahi kukupenda wewe kimapenzi, nilikuchukulia kama rafiki ndo mana sijawahi kuzungumza na wewe swala la mapenzi. mimi huwa nikikipenda kitu sichukui muda ninasema hapo hapo. tangu nikufahamu wewe tuna miezi kama mitatu sijawahi hata kukushika nywele. kama kuna kitu nimekifanya kwako ni kukushka mkono tu kitu ambacho hata marafiki wanakifanya. Sikuwahi hata kukuleta kwangu kwa kuwa najua ni mke pekee ndiye anaestahil kupajua nyumbani kwangu.
dada huku akilia akamwambia mbona ulikua unanihonga???
yule kaka akacheka akasema.
sikuwahi kukuhonga mimi nilikua nakupa tu kama rafiki yangu. hata marafiki zangu wa kiume huwa nawapa kwa sababu nimepewa na nilichokitoa hakiathiri uchumi wangu. sikuona sababu ya kukunyima angali ninacho. Sijafundishwa hivyo na usidhani pindi nitakapo muoa rafiki yako wewe ukiniomba kitu nitakunyima. hapana nitakupa kama ninacho ila katu sitokupa kipaumbele tena kuliko mke wangu. mke wangu akiridhika kwa nilichompa basi nawe utapata.
bas yule dada akamwambia siwezi kumwambia kwakua rafiki zangu watanicheka mnooo wote wanajua wewe ni bwana wangu. siwezi naomba unipende mimi.
yule kaka akamwambia siwezi kukupenda wewe kama mke wangu. sina hisia hizo kwako. na usiogope kumwambia ni bora ukaseme wajue wewe uliuelewa upendo wangu vibaya watakubembeleza na kukufariji, kuliko kukaa kimya. maana mimi nitakapokutana na rafiki yako popote nitamwambia tija ya moyo wangu nae atakapo nikataa kwa kudhany mimi ni shemeji yake nitamuelewesha jinsi gani mimi na wewe tulivyo na ili kujitetea na kumpata nimpendae nitaingia ndani zaidi na kumweleza kuwa nilikutuma wewe ujumbe huu na hukuufikisha. hapi ndipo rafiki zako watakudharau na kukukebehi. watakuletea maringo ya waziwazi na kukucheka. utajiona huna thaman. kuelewa vibaya sio tatzo, ila tatizo linakuja pale ulipogundua kuwa ulichokielewa sicho nawe ukang'ang'ania.
Yule dada akamjibu sasa kwanini hukunipenda mimi wakati ndio ulitangulia kuniona?
yule kaka akamjibu co kila kilichopo mwanzo kinastahili kuna vingne vyenye kufaa vipo kati na hata mwisho... kikubwa usiwe na haraka katika kufanya maamuzi. Nikuulize swali dada????
yule dada akamjibu ndio niulize.
yule kaka akamwambia hapo ulipo una usichana wako?
yule dada akamjibu hapana.
kaka akamuuliza ni nan alieutoa?
yule dada akamjibu mpenzi wangu wa kwanza.
yule kaka akamuuliza yupo hai au amekufa??
yule dada akamwambia yupo hai na kwa sasa ana mpenz wake mwngne.
basi yule kaka akamwambia
KWANINI HUKULAZIMISHA NDOA KWA MTU ALIYETANGULIA KUUJUA UNDANI WA MWILI WAKO NA UJE KULAZIMISHA NDOA KWANGU MIMI MTU NILIYETANGULIA KUZIJUA TAMAA ZAKO????
rafiki yako alikua mstaarabu sana kati ya marafiki zako wote, hakunywa pombe, hakupenda mziki. mlimlazimisha tu kuja. mara nyingi alikua ni mtu wa kukaa chini, mara kwa mara alisisitiza tirudi nyumban. hata tulivyokua tukiondoka alinambia ni vema na wewe uende ukupumzike maana umechoka pia. Sisi nyumbani tutakwenda wenyewe sio mbali na hapa tukichukua taxi. wenzake wote walimbeza na kumwabia ebuuuuu huko hiyo ndo kazi ya mwanaume tupeleke sie shemeji utupe na hela ya supu kesho. hivi mlimpata wapi rafiki kama yule? mbona haendani na ninyi?
yule msichana huku akilia akajibu, yule ni house girl wetu huwa napenda kutoka nae ili baba na mama wasihisi nakwenda kufanya mabaya huko niendako.
bas yule kaka akamwambia nenda kamwambie house girl wenu kuwa NAMPENDA SANA, AJE NYUMBANI KWANGU AFANYE KAZI YA KUNIPENDA KWA DHATI NAMI NITAMLIPA UPENDO.
NB: Hakuna Mwanaume anayependa kuoa mwanamke mpenda starehe. maana anajua huyo hawezi kuwa mama mwema wa watoto wake.
Hakuna mwanaume anayependa kuoa Mwanamke mwenye matumizi makubwa ya pesa. kwakua anajua huyo hatomfanya afikishe malengo wake.
Hakuna mwanaume anayependa mke wake awe mtu wa makundi. maana anajua kua hawezi kuwa na maadili yanayofaa.
Ewe mwanamke, Mwanaume anayekupenda ukiwa kwenye kimini na safari za Club na kila maeneo yenye Anasa za kidunia. huyo si mwanaume muoaji. bali anaufanya mwili wako kama starehe yake pia. yaani Bia starehe na mwili wako ni sehemu ya starehe.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz