TENDO LA NDOA NA UMUHIMU WAKE KATIKA NDOA* - EDUSPORTSTZ

Latest

TENDO LA NDOA NA UMUHIMU WAKE KATIKA NDOA*

Matokeo ya KUSHANGAZA ya uchunguzi wa wanawake 1,000! ▷ Tuko.co.ke
.💞 _Kuwepo na mapenzi ya dhati kati ya wanandoa hufanya mambo mengi kuwa rahisi na mepesi bila kujalisha ni kipindi cha furaha au majonzi; sababu inakuwa upo na mtu ambaye anakufanyia unafuu wa mhusika kuamini kuwa kila kitu hatimaye kitakuwa sawa mradi huyo mpenzi wako yupo karibu na wewe anakupenda na mnashirikiana vilivyo kwa kujaliana kwa misingi ya ‘Chake changu, changu chake’_.....✍🏽
..💞 *Mapenzi na kufanya mapenzi baina ya wawili wapendanao* _hasa kama wameoana ni moja ya chachu ya ndoa ambayo husaidia kushikilia na kuimarisha ndoa hiyo endapo ikatumika vizuri na kwa wote kufurahia hasa kwa wale ambao hushirikiana katika kila kitu._...✍🏽
*💞Siri ya kufurahia tendo la ndoa ni wanandoa wote* _kuridhika na utendaji wa mwenza wao hasa wakati wa tukio, kwa kujituma, kuwa mbunifu, kutaka na kufurahia tendo hilo_. Ingawa ni kweli kwa nadra inaweza tokea mwenzako akawa na hamu na wewe usiwe nayo (ikitokea mara chache sana – hili linaeleweka, na linaweza kukubalika ila si kwa kuzoea na ikawa utamaduni; iwe kwa mwanaume ama mwanamke) .....✍🏽
*💞Izingatiwe kuwa, kufurahia tendo la ndoa haiji kirahisi rahisi…* _Mazingira ya kufurahia tendo hili muhimu ni lazima yajengwe na yaimarishwe mara kwa mara._ Maana ni wazi kuwa uhai wa kila ambalo linatakiwa kuishi ni lazima litunzwe kwa umakini na kujali. _Hivyo kufurahia tendo la ndoa pia hupaswa kuimarishwa kwa nilivyotaja hapo awali – Kupenda, kujituma, utundu, maarifa na Ubunifu._ Na haya yote huwa rahisi sana ikiwa mwanandoa wako wampenda ama kumkubali, na kubwa kuliko ikiwa na yeye pia hujituma, ‘ni mtundu’ na ana maarifa pia.....✍🏽
*💞Hivi vitu (Kujituma, utundu, maarifa na ubunifu) haviji hivi hivi pia …* _Na ndio kwa misingi hiyo wanandoa hushauriwa kuzungumzia tendo la ndoa, kama haridhiki katika tendo, kitu kipi hupendi, kitu gani unapenda, wapi unapenda kuguswa, vipi unapenda kukunwa, na ni kitu gani ambacho kinakupandisha mzuka – huku wewe mwenzie ukiwa mtundu katika kuhakikisha unavumbua maeneo mengine ambayo hata yeye hakujua kuwa anaweza pata raha hiyo ambayo anaipata kwa wakati huo (TAHADHARI – Yapaswa kuwa na mipaka pia)._....✍🏽
‬: *💞Mnaweza msiwe kila mmoja si mtaalam kwa mwenzie..* _mnapoanza mahusiano yenu ya mapenzi, ila inapaswa na ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha ufundi huo unaongezeka kadri siku zinavyozidi kwenda kwa mwenza wake huyo na si kupungua. Izingatiwe pia kuwa, huonyesha ili kujua mnafurahia, msingi ni kutafuta rhyme ambayo huwafanya wote mfurahie tendo hilo la ndoa na kuwafanya kuwa na kiu juu ya mwenza wako pale unapokuwa umemkosa_...✍🏽
*💞Ndoa si kufanya tu Mapenzi ni zaidi ya hapo,* _ila mwisho wa siku kufanya Mapenzi ni muhimu mno kwa ustawi wa ndoa kati ya wanandoa. Ni suala ambalo kiharaka haraka linaweza chukuliwa kwa wepesi, ila mwisho wa siku lina faida sana_...✍🏽
*FAIDA YA TENDO LA NDOA KWA WANANDOA*
....💞 *_Linajenga ukaribu zaidi kwa wanandoa._* _Tokana na majukumu ya kifamilia ambayo yanaenda yakikua kwa kasi na kufanya baadhi ya wanandoa kutokuwa na wakati wa kuwa karibu zaidi kunakuwa na muda mchache kwa baadhi kubadilishana mawazo. Wanandoa wengine wamefaulu kwa kuhakikisha kila siku/au mara kadhaa kwa juma kujulishana habari zao wanapokuwa hawapo pamoja. Tendo la ndoa linaweza tumika kama wakati muafaka wa kila mmoja kutiririka na kuongea mambo mbalimbali na hata kupanga mipango yenu ya kimaisha. Hilo hutokea pale mnapokuwa mnataka kujianda, nusu fainali au baada ya mchezo kuisha tegemeana na mtiririko wenu upo vipi._.....✍🏽
💞 *_Kumwelewa Mwenzi wako_*
_Tendo la ndoa lina lugha yake… Tendo hili haliishi tu katika kufurahia na kufika kileleni bali pia linasaidia kumwelewa na kumsoma mwenzi wako. Ndio maana ni vema sana kumjulia mwenza wako kitabia na mwenendo kwa kuhusisha tendo hilo. 💞 Ikiwa wenza mna tabia ya kushirikiana na kuhusishana katika masuala ya kila siku ni rahisi kutambua kuwa mwenza wako siku hiyo kachoka, kachukizwa (iwe na wewe ama mtu mwingine), ana mawazo, ana wasiwasi, hana raha n.k._
.....💞 _Haijalishi kuwa mwenza wako yupo katika hali ipi wengi hujitahidi hilo lisiwe kikwazo kwa tendo la ndoa (hasa wanaume) _ 💞 Hivyo ni rahisi kumjulia tokana na namna mnavyokuwa faragha kujua kuna jambo ama la. Ni wazi wakati mwingine kunaweza kuwa na jambo na mwenzi wako asikuhusishe, kupitia tendo la ndoa unaweza pata viashiria._....✍🏽
‬: 💞 *_Inasaidia wanandoa kupata Watoto_*
... _Watoto wana raha yake katika ndoa, na wana nafasi kubwa sana katika kuweza kuimarisha ndoa, kuleta furaha katika familia, kuwajenga na kuwa komaza kama wazazi na pia kuwaunganisha zaidi wanandoa kama mwili mmoja. Si wote wamejaaliwa kupata watoto (my heart goes out to them)_ – _ila ukweli ni kuwa mara nyingi hiki ni kipengele muhimu katika ndoa ambacho wanandoa wenyewe na jamii hutarajia kuwa muhimu kufanikisha ili ndoa ionekane kuwa ina mafanikio. 💞💞Niongeze kuwa tumepishana kutafsiri mafanikio ni nini katika ndoa, ila wengi huwa na msimamo wa kuwa watoto ni muhimu katika ndoa_....✍🏽
‬: 💞 *_Kumwelewa Mwenzi wako_*

‬: 💞 *_Kutatua ugomvi/mgogoro kati ya wenza_*
..... _Ugomvi haukwepeki hata kama mwapendana vipi (ingawa frequency ya ugomvi hupishana kati ya wanandoa). Tendo la ndoa linazungumza mambo mengi sana…. Kitendo cha kukutana kimwili na mwenza wako kwa namna moja wapo inakuwa ni akili na mwili wako kukubali kuwa umejitoa kwa mwenzi wako kwa wakati huo. Kuna makabila ambayo hata uwe umegombana vipi na mke/mume wako, ikitokea tu ukalala naye na kufanya tendo la ndoa haijalishi kosa lilikuwa ni lipi inachukuliwa limesamehewa na yapaswa kusahau na kusonga mbele_.....✍🏽
💞 *_Kupunguza uchovu/Msongo wa mawazo_*
..... _Ndoa ni moja ya njia kwa baadhi kuweza kupunguza uchovu alionao na kwa wengine hata msongo wa mawazo. Tendo likifanywa vema na kwa ustadi, huweza kumwondolea mwenzi wako uchovu au msongo wa mawazo kwa kiwango kikubwa. Unafuu huo utegemea lakini, wengine inakuwa tu unafuu wakati wa tendo hilo na hali wengine hupata nafuu ya muda mrefu. Hivyo ikiwa mwenzi wako yupo katika hali hiyo katika kutafuta namna ya kuhakikisha anapata unafuu, unaweza tumia tendo la ndoa kama silaha ya kumrudisha mwenzi wako katika hali nzuri_.......✍🏽
💞 *_Linajenga heshima ndani ya ndoa (hasa kwa wanaume)_*
..... _Hili linawezekana pande zote (mke na mume) mmelipa umuhimu wa pekee tendo la ndoa hadi mkiwa faragha wote hufurahia tendo hili hadi kuna wakati mwajihisi mpo mwili mmoja kama si ndani ya ngozi moja. Tunarudi palepale, kuwa ni muhimu ukampenda mtu wako, ukapenda hilo tendo, mengine yanafuata mkiwa faraghani...._✍🏽
‬: 💞 *_Linatumika kupata unachotaka/Kulaghai (hasa kwa wanawake)_*
.... _Hili linategemea unalifanya kwa namna ipi… Ukilifanya kana kwamba ni hongo ya lazima na kuwa wamaanisha hutokubali kuwa faragha bila kutimiziwa kitu Fulani – Hapo inakuwa ni tatizo na ndio ulaghai wenyewe. Ila lifanywapo kwa upendo, utani wa kimapenzi, kwa kutoa maneno matamu na kubembembeleza, husaidia kuongeza ashiki kwa wapenzi (inaweza isiwe kwa wote) na huku pia ukifanikiwa kupata kile ambacho unataka mwenzio akiwa katika mood nzuri_....✍🏽
🌺🌺 *Mwisho*🌺🌺
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz