♥: *NJIA 4 ZA KUZUIA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO* - EDUSPORTSTZ

Latest

♥: *NJIA 4 ZA KUZUIA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO*

Hizi ndio faida za kumkumbatia mumeo/mkeo – MINYAtz
💗💗💗💗💗💗💗💗💗
```Migogoro katika mahusiano ya mapenzi ni kitu cha kawaida kutokea.
Wenza katika mahusiano hugombana na ugomvi mwingine hupelekea hadi kupigana na kusababishiana maumivu hata kuumizana.
Lakini migogoro mingi inaweza kuepukika kama tu wenza hao wakitambua vitu vinavyosababisha kugombana kwao na kuweka mikakati itakayowasaidia kuishi kwa amani zaidi na kuifuata.```
🌹🌹
💗💗💗💗💗💗💗💗💗```Mara nyingi katika mahusiano ugomvi hausababishwi na ujumbe au mawazo tofauti yanayotolewa na mmoja wao bali namna ujumbe huo unavyotolewa na jinsi mpokeaji anavyotafsiri.
Hii inamaana kuwa kama wenza hao wakikubaliana na wakawasiliana hoja zao katika namna ambavyo kila mmoja wao anahisi kusikilizwa na kujaliwa namba za magomvi zitapungua sana.
Hebu tuone namna ambavyo migogoro katika mahusiano inaweza kupunguzwa na kusuluhishwa:```
🌹🌹
: *1: Acha Kujihami*
```Mapambano kati ya wenza wawili yanaweza kufananishwa na mpambano wa mchezo wa ngumi.
Bondia mmoja anapotupa makonde mfululizo na mwingine anajaribu kuzuia ni kawaida atakuwa narudi nyuma na kuruhusu mwenzake aendelee kumvamia.
Vivyo hivyo katika ugomvi katika mahusiano ya wapenzi.
Mwenza mmoja napomvamia mwenzake kwa maneno makali na tuhuma kwa mfano, na mwingine akawa anajihami nayo kwa kupinga au kwa kurudisha tuhuma, kinachotokea ni kuwa mapambano yataendelea.```
🌹🌹
💗💗💗💗💗💗💗💗💗
```Kama unatengeneza mazingira ya kujihami na mpenzi wako basi unafanya aendelee kukushambulia na hivyo kuendeleza mgogoro kwa muda mrefu.
Zuia kujihami na toka katika uringo wa mapambano.
Kumbuka bondia hawezi kupigana na upepo, kama hakuna mpinzani basi hakuna pambano.
Epuka majibizano ya maneno ambayo yatapelekea ugomvi.
Kuwa wa kwanza kukaa kimya, ikiwezekana kuondoka kwa muda huo na muendelee mazungumzo baadae wakati kuna utulivu na kusikilizana.```
💗💗💗💗💗💗💗💗💗
```Pia inaonyesha kuwa unajali.
Mpenzi yeyote anapenda kuona kuwa mawazo yake na yeye mwenyewe yanajaliwa.
Unaporudia kutamka alichosema kuna maana mbili, ya kwanza ni kuwa umemsikia vizuri lakini pili ni kuwa inaonyesha kuwa unajali.```
Mfano: *“Najua jambo hili ni muhimu kwako, lakini nafikiri tungeangalia mambo yanayohusu watoto na mahitaji yao kwanza na hilo lifanyike baade”*
```Jaribu mbinu hii kwa mwenza wako mnapokuwa na migogoro na uone jinsi inavyofanya maajabu.
Kumbuka sauti inayotumika iwe yenye kuonyesha kujali na sio kuongea kama vile ni polisi.```
🌹🌹




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz