NAOMBA NIKWAMBIE JAMBO HILI MUHIMU KWENYE MAISHA, LITAKUSAIDIA SANA. - EDUSPORTSTZ

Latest

NAOMBA NIKWAMBIE JAMBO HILI MUHIMU KWENYE MAISHA, LITAKUSAIDIA SANA.

Chochote ulichonacho leo hii, usisubiri mpaka kikuponyoke ndipo uanze kujuta. Maana, utakapoanza kupay attention ndipo kitakuwa kishakuondoka na hakirudi tena.
Unae mama? Mueleze kuwa unampenda, mthamini na mtunze. Maana, wakati wewe unasheherekea mothers' day, siku hiyo hiyo mtu mwingine anamzika mama yake. Vivyo hivyo hata kwa baba.
Unae Mke/Mume/girlfriend/Boyfriend? Mpende, tambua thamani yake katika maisha yako kwa sababu wakati mtu mwingine akisheherekea Valentine day na mpenzi wake, mwingine anamkumbuka mpenzi wake aliempoteza.
Ishi maisha yako sasa! Furahia kila sekunde ya uhai uliyopewa na Mwenyezi MUNGU. Pale utakapotizama nyuma isiwe ni majuto, bali iwe ni shukrani kwa hatua kubwa uliyopiga.
ITUNZE NDOA YAKO"
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz