My future wife Nakuahidi yafuatayo... - EDUSPORTSTZ

Latest

My future wife Nakuahidi yafuatayo...


1. Nitakuangalia machoni mara kwa mara na kukuhakishia mapenzi niliyonayo juu yako.
2. Nitaendelea Kukupenda na kukujali kwa kila hali na kukuhakikishia unalo bega langu la kuinamia.
3. Nitapitiliza migahawa yote mizuri, sitaingia kununua chakula hata kama nina njaa ili tu, nile chakula chako ulichoniandalia nyumbani.
4. Nitaingia kuoga na wewe atleast kila kutakapokuwa na nafasi, jiandae kwa hilo na naomba usiniulize ni nini kitakachokua kikitokea humo bafuni.
5. Nitakufanyia massage kipindi ukiwa mjamzito whether you need a massage or not.
6. Nitajitahidi kuendelea kuwa muaminifu licha ya vikwazo na vishawishi vingi vilivyopo mbele yangu!
7. Nitaku-suprise kwa kukukumbatia wakati ukiwa jikoni unaosha vyombo!
8. Nitaingia jikoni kimya kimya na kukuangalia unavyopika, na nitakusaidia kupika pale utakaponiona!
9. Siku zote ntakusubiri wewe kabla sijaanza kula, ili tule pamoja katika sahani moja!
10. Nitakutazama kwa namna ya ajabu kila wakati, nitakuombea na kumshukuru Mungu kwa zawadi ya kunipa mke mwema uliye mbele ya macho yangu!
Najua umeshaambiwa na kusikia kwamba ati Christian Black brothers hawako romantic, kwamba ni washamba na boring. Subiri uone..utaamini kwamba hayo madai sio ya kweli...
Dear future wife Yote haya yatawezekana endapo;
1. Utakua mtiifu kwangu, mvumilivu, ukaniheshimu, kunisikiliza na kunitia moyo na kuniombea.
2. Utaniacha nitumie mamlaka yangu ya kichwa cha nyumba pasipo kunipanda kichwani.
3. Utanisikiliza, utakua mwaminifu na kuridhika na mimi kwa kila hali nitakayopitia.
4. Utajiweka katika hali nzuri, kuanzia mavazi, mwili, na hata nyumba yetu!
5. Utakua mwakilishi wangu mwema asie na mashaka yoyote katika mambo yote kwa sababu wewe ndio mimi, mimi ndio wewe ukiharibu wewe nimeharibu mimi.
Ukizingatia hayo we will live happily ever after!!
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz