Kuna Wanawake Wengi Sana Ambao Wana Ndoto Kubwa na Wana Uwezo Mkubwa Sana Ila Kikwazo kikubwa ni KUKOSA KUJIAMINI.

Kuna Wanawake Wengi Sana Ambao Wana Ndoto Kubwa na Wana Uwezo Mkubwa Sana Ila Kikwazo kikubwa ni KUKOSA KUJIAMINI.
Inawezekana umepitia MAISHA MAGUMU SANA na Baba yako alikukataa ulipozaliwa.
Hali hiyo imekusababisha MAISHA YAKO yote ujione ni mtu usiyekubalika na Usiye na thamani maishani mwako.
NAKUKUMBUSHA kuwa Thamani yako ni Kubwa mno na ndio maana Mungu aliruhusu UZALIWE.
Usikubali KUJIONA hauwezi kwa sababu hiyo.
Umepitia MAUMIVU MAKALI sana siku za hivi karibuni.
Umeumizwa na mtu wa karibu sana na imekufanya uwe na Usiku wa Vilio mara kwa mara.
Kumbuka unayo nafasi ya kufungua ukurasa mpya.
Hata kama umepitia jambo gumu kiasi gani, bado unayo fursa ya kufurahia MAISHA tena.
Wakati mwingine inabidi ukubali kusamehe, kusahau na kuachilia yaliyopita ili UANZE UKURASA MPYA.
Kumbuka kuwa ukitupa DHAHABU kwenye zizi la NG’OMBE wataikanyaga na kuidharau kwa sababu hawajui thamani yake ingawa HAIMAANISHI haina thamani.
Wengi waliokutendea mabaya kuna siku watajua walikuwa wanacheza na DHAHABU.
Mapito mengine ni kwa ajili ya kukusaidia kujenga misuli ya MAISHA na kukuandaa uwe Msaada kwa wengine, TAKE IT POSITIVE.
Unaishi na mtu ambaye kila wakati anakuambia “HAUWEZI”,
.
”HAUTAFIKA MBALI” nk..
Isikuvunje moyo.
Wanaweza kutoamini Ndoto YAKO bali hawawezi kukataa MATOKEO YAKO.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post