Mwaka 2020 umebadilisha mtazamo mzima, umebadilisha kabisa mwelekeo mzima wa maisha yetu. - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwaka 2020 umebadilisha mtazamo mzima, umebadilisha kabisa mwelekeo mzima wa maisha yetu.


Mavellah TZ - MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU ...

\Mwanzoni mwa mwaka huu tuliona bei ya nyanya ikipanda kwa kiwango kisichomithilika. Nyanya ilikuwa Lulu. Na tukasema imepambana mpaka kufikia bei ya tufaa.
Na kuna barakoa. Msamiati huu umekuwa maarufu sana mwaka huu. Sio kwamba ni kitu kigeni. La! Tumezoea kutumia "Mask." Ni mwaka huu ambapo tumevaa barakoa karibu dunia nzima.
Ni mwaka huu huu ambapo tumeona watu wakigombania 'vitakasa' na 'chachi' madukani. Ndio! hii sio misamiati migeni pia. Ni "sanitizer" na "toilet paper." Tumezoea kuona vyakula kama mkate au maji vikigombaniwa au kuuzwa kwa bei ya juu. Na sio kitakasa au chachi. Ni ajabu sana.
Jambo jingine la pekee mwaka huu ni 'kujitenga nyumbani' maarufu 'social distancing.' Nafahamu kujitenga sio kitu kigeni kwa mamilioni ya vijana wa kitanzania wasio na ajira. Simu; Bip! Bip! Haloo Shemeji! Rimoti ipo wapi? Kipindi ninachokipenda cha luninga sasa kinaoneshwa kutokea nyumbani. Hii ni kwa hisani ya kirusi cha kovid -19 almaarufu korona.
Hoja yangu ni kuwa vile vitu tulivyochukulia poa kabisa ndio vinatushangaza. Ona bei ya nyanya. Mtu wa karibu zaidi kwenye familia, unaemuona kila siku, mnaezungumza, unaempenda na kumuamini ndio anafanya jambo linalokushangaza.
Na mtu huyo anafanya jambo hilo mbele ya macho yako na huoni. Jambo ambalo unapaswa kabisa kuliona na kulizuia linatokea. Na linatokea nyumbani lakini linakupita. Yule anayefanyiwa anajaribu kukupa kila ishara lakini wapi. Ni kama chachi, ni kama toilet paper. Ni muhimu. Tunaiona na nakuitumia kila siku, lakini... Baada ya janga tunakurupuka na tunaona kumbe tuko nazo kila siku.
Tunafahamu barakoa inatumiwa na wahudumu wa afya, watu wenye tatizo la kiafya na wakati wa dharura au janga. Lakini kwa kipindi kirefu, kama jamii, tumevaa barakoa inayofunika mdomo, pua mpaka macho na masikio yetu kwenye jambo ambalo hatupaswi kufanya hivyo.
Tunaitumia barakoa kila siku kufunika nyuso zetu tusione, tusitazame, tusichukue hatua kushughulikia unyanyasaji wa watoto kingono nyumbani, mtaani na shuleni. Tunatumia barakoa kuwa kimya, kuona aibu, kutozungumzia na kunyanyapaa.
Endelea kwenye comments 👇 share
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz