MUDA SAHIHI WA MAMA ALIYEJIFUNGUA KUANZA TENA TENDO LA NDOA - EDUSPORTSTZ

Latest

MUDA SAHIHI WA MAMA ALIYEJIFUNGUA KUANZA TENA TENDO LA NDOA


Kipindi cha kunyonyesha ni kipindi kigumu sana kwa mama kwani huambatana na uchovu mwingi unaotokana na kuongezeka kwa majukumu ya kumhudumia mtoto mchanga ambayo huchangia kwa mama kutokuwa katika hali nzuri ya kufikiria kufanya tendo la ndoa
Baada ya kujifungua, wanawake wengi hawaoni tendo la ndoa kama ni muhimu sana kwao hata kufikia hatua ya kutojali hisia za wenza wao. Mwanamke anapojifungua huwa na kidonda, mchubuko na hata kuchoka kwenye sehemu za tupu yake kama atakuwa amejifungua kwa njia ya kawaida.

Kwa aliyejufungua kwa njia ya upasuaji, mama huyu huwa na kidonda kinachotokana na upasuaji kwenye tumbo lake na kwenye mfuko wa kizazi

Je ni muda gani sahihi kwa mama aliyejifungua kuanza tena kujamiana?
Kitaalamu mama aliyejifungua hushauriwa kusubiri mpaka wiki sita (baada ya kuanza kliniki- postnatal clinic) ndio aweze tena kufanya tendo la ndoa.

Kuzaa huathiri vipi tendo la ndoa?
Kipindi cha kupona baada ya kujifungua hutegemea na njia ya kujifungua aliyotumia mama.

Kwa wale ambao wakati wa kujifungua waliongezewa njia kwa ajili ya kurahisisha kupita kwa mtoto (Episiotomy) au walichanika (Tear) na kushonwa, nyuzi hupotea baada ya siku 10 mwilini na wiki mbili za ziada mpaka michibuko na kidonda/vidonda kupona kabisa. Mama huyu anashauriwa kufanya staili (wakati wa kujamiana) ambazo zitapunguza kuegemewa kwa sehemu ya mshono. Staili ambazo mama hulazimika kunyanyua miguu au kukunja miguu mpaka kwenye kitovu chake ni bora akaziepuka. Anatakiwa kuwa muangalifu sana wakati wa kujamiana pamoja na kufanya tendo la ndoa kwa taratibu (slow and gentle).

Kwa mama aliyejifungua kwa njia ya kawaida (Spontaneous Vaginal Delivery, SVD) pasipo kuongezewa njia au kuchanika, kupona kwake ni haraka na anaweza kuanza tena kufanya tendo la ndoa mara tu damu inayotoka (Lochia) kuacha, mara nyingi damu hii kutoka huacha kabisa ndani ya wiki nne hadi wiki sita.

Mama aliyejifungua kwa njia ya upasuaji (Caesarean section) huwa na wasiwasi , hofu kutokana na kidonda cha upasuaji, hivyo ni vyema kwa mama huyu kusubiri mpaka nyuzi kutoka kabla ya kufanya tendo la ndoa na pia azingatie kufanya kwa utaratibu (gentle).Staili zitakazoongeza kugandamizwa kwa eneo la mshono ni bora akaziepuka.


Je, kunyonyesha huathiri tendo la ndoa?
Baada ya mama kujifungua, kunakuwepo na mabadiliko ya viwango vya vichocheo mwilini mwake ambavyo ni; 
Kupungua kwa kiwango cha Oestrogen-Kupungua kwa homoni hii husababisha; 
Mama kupata kinga dhidi ya kushika tena ujauzito ndani ya muda mfupi kwa kumzuia kuingia katika hatua ya ovulation. 
Ukavu kwenye tupu ya mwanamke (Dryness of vagina) kwa baadhi ya wanawake 
Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa na hata kukosa msisimko kwenye kisime (Low clitoris sensation). 
Kupungua kwa kiwango cha kichocheo aina ya testerone pia husababisha kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa. 
Kuongezeka kwa kiwango cha homoni aina ya Prolactin (ambacho pia hupatikana kwenye maziwa ya mama) husababisha mama kujihisi hali ya kuridhika kimapenzi. 


Zifuatazo ni sababu za mama kupoteza hamu ya tendo la ndoa baada ya kujifungua: 
Uchovu—Kutokana na kuongezea kwa majukumu ya kumlea na kumhudumia mtoto 
Mabadiliko ya muonekano wa mwili-Kina mama wengi baada ya kujifungua hupoteza hali ya kujiamini kutokana na mabadiliko ya mwili kama kuongezeka uzito, matiti kuwa makubwa na hata kubadilika muonekano wa matiti yao, kubadilika shepu nk. Na hivyo kuchangia kupoteza hamu ya tendo la ndoa 
Wasiwasi au hofu kuwa tendo la ndoa linaweza kuleta maumivu baada ya kujifungua 
Kuogopa kushika ujauzito tena mara tu baada ya kujifungua 
Ukavu kwenye tupu ya mwanamke kutokana na kupungua kwa homoni aina ya oestrogen (hutokea kwa baadhi ya wanawake) 
Hali ya kuridhika kimapenzi kutokana na homoni ya Prolactin 
Kupungua kwa kichocheoa aina ya Testerone 


Mambo ya kuzingatia Kwa mama aliyejifungua kabla ya kufanya tendo la ndoa tena 
Mama anahitaji kuzungumza na baba mtoto na kumueleza ukweli kuhusu hisia zake juu ya tendo la ndoa 
Baba anashauriwa kuwa mvumilivu kama mama bado anapata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa kwani hali hii ni ya muda tu 
Kumsaidia na kumpa ushirikiano mama katika kulea na kumtunza mtoto ili apate muda wa kupumzika na hivyo kuongeza utayari wa mama katika kufanya tendo la ndoa 
Kumpenda, kumjali na kumjengea mama uwezo wa kujiamini kutokana na mabadiliko ya mwili wake yaliyotokana na ujauzito (kuongezeka uzito, kubadilika muonekano wa matiti, shepu nk) 
Mama anashauriwa kuweka mazingira mazuri ya kukutana kimwili na baba mtoto kwani hata yeye bado anamuhitaji katika kipindi hiki. 
Kuchagua muda mzuri usiokuwa na usumbufu wowote ule kutoka kwa mtoto (muda mzuri ni baada ya kumnyonyesha mtoto) 
Mama anatakiwa kujikagua na kujichunguza kwenye tupu yake taratibu kwa kutumia vidole vyake ili aweze kufahamu kama anaweza kupata maumivu wakati wa kujamiana 


Kama unaendelea kupata maumivu, au uke kuwa mkavu sana ni vyema kumuona daktari kwa ajili ya ushauri na matibabu
Kipindi hiki cha wiki sita ni muhimu sana kwa mama kuwa karibu sana mwenza wake na kumpa ushirikiano mpaka wote watakapo kuwa tayari kwa tendo la ndoa.
Ni vyema kutumia njia za uzazi wa mpango hata kama unanyonyesha kwani unaweza kushika mimba usiyoitarajia, mimba hizi nyingi zimepatikana katika kipindi hiki.
Kama bado mnaona hampo tayari kwa tendo la ndoa, ni vyema kuendeleza mapenzi mubashara kama kupigana busu, kutomasana, kukumbatiana, kupapasana sehemu tofauti za mwili ili hisia za tendo la ndoa zirudi kama hapo awali





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz