Mambo ya Kujifunza Wadada Kabla ya Kuingia Kwenye Mahusiano. - EDUSPORTSTZ

Latest

Mambo ya Kujifunza Wadada Kabla ya Kuingia Kwenye Mahusiano.

Kuna mdada alikutana na mkaka wakat wako safarini, yule kaka akamuomba mdada namba ya simu njian akamnunulia kila kitu alichotaka, alipofika stand mkaka akamlipia usafiri mpaka home kwao alikokuwa abaelekea. Basi wakawa wanawasiliana kila siku. Siku nyingne anamuita wanatoka wanakula na kunywa na hela anampa.

Yule dada akawaambia marafiki zake nimepata bonge la bwana jamani nitake nini mimi nisipewe? mashoga wakamwambia weeee embu jaribu yule dada akampigia yule jamaa simu akamwambia leo nipo nipo tu natamani kutoka ila sina hela ya saloon nimemisi sana kwenda Club na marafiki zangu.

Yule jamaa akamwambia ok akamtumia laki 3 ya saloon na kumwambia kama isipimtosha aseme.

Wenzie wakasema lol shoga bwana umempata. ilipofika jioni yula mwanaume akapiga simu kwa yule binti akamuuliza Club gani mnakwenda? yule dada akataja Club wanayotaka kwenda yule bwana akamwabia basi namtuma mtu aje awachukue mie mtanikuta huko.

Baada ya muda yule dada akaenda yeye na jopo lake, walipofika wakanywa, wakala na kucheza. wakarudishwa home kama walivyoahidiwa. Siku ya pili yule bwana akamwambia yule dada nataka kuzungumza na wewe ila please njoo peke yako. Yule dada akajikoki akaenda alipofika kule yule kaka akamwambia nimempenda sana rafiki yako yule mweupe mweupe naomba ukamwambia hisia zangu hizi wala sina plan ya kumchezea nitamuoa kabisa

Sikuwahi hata kukuleta kwangu kwa kuwa najua ni mke pekee ndie anaestahil kupajua nyumbani kwangu.


Yule dada akamwambia mimi je? yule kaka akamuuliza wewe nini? yule dada akamjibu mimi utanipeleka wapi kwa hiyo mimi ndo unaniacha? yule kaka akamwambia mimi sikuwahi kukupenda wewe kimapenzi, nilikuchukulia kama
 rafiki yangu ndo mana sijawhi kuzungumza na wewe swala la mapenzi mimi huwa nikikipenda kitu sichukui muda ninasema hapo hapo.

Tangu nikufahamu wewe tuna miezi kama mitatu sijawahi hata kukushika nywele. Kama kunakitu nimekifanya kwako ni kukushika mkono tu kitu ambacho hata marafiki wanakifanya

Dada huku akilia akamwambia mbona ulikua unanihonga? yule kaka akacheka akasema sikuwahi kukuhonga mimi nilikua nakupa kama rafiki yangu.

Sina sababu ya kukunyima angali ninacho sijafundishwa hivyo na usidhani kama nitamuoa rafiki yako halafu wewe ukiniomba nitakunyima hapana nitakupa kama ninacho ila katu sitokupa kipaumbele kuliko mke wangu.

Mke wangu akiridhika kwa nilichompa basi nawe utapata.
Basi yule dada akamwambia siwezi kumwambia rafiki yangu watanicheka mnooo wote wanajua wewe ni bwana wangu. Siwezi naomba unipende mimi kaka yangu.

Yule kaka akamwambia siwezi kukupenda wewe kama mke wangu sina hisia hizo kwako, na usiogope kumwambia ni bora ukaseme wajue wewe uliuelewa upendo wangu vibaya watakubembeleza na kukufariji, kuliko kukaa kimya.

Maana mimi nitakapokutana na rafiki yako popote nitamwambia haja ya moyo wangu nae atakapo nikataa kwa kudhani mimi ni shemeji yake nitamuelewesha jinsi gani mimi tulivyo na ili kujitetea ili kumpata nimpwndae nitaingia ndani zaidi na kumweleza kuwa nilikutuma wewe ujumbe huu na hukuufikisha. hapo ndipo rafiki zako watakudharau na kukukebehi. Watakuletea maringo ya wazi wazi na utajiona huna thamani. Kuelewa vibaya sioo taitzo ila tatizo linakuja pale ulipogundua kuwa ulichokielewa sicho nawe ukang'ang'ania.

Yule dada akamjibu sasa kwanini hukunipenda mimi wakati ndo ulitangulia kuniona? yule kaka akamjibu sii kila kilichopo mwanzo kinastahili kuna vingine vyenye kufaa vipo kati na hata mwisho pia. Kikubwa usiwe na haraka katika kufanya maamuzi nikuulize swali dada? yule dada akamjibu ndio niulize. Yule kaka akamwambia hapo ulipo unausichana wako? yule dada akamjibu hapana. Kaka akamuuliza ni nani alieutoa? yule dada akamjibu mpenzi wangu wa kwanza. Yule kaka akamuuliza yupo hai au amekufa? Yule dada

akamwambia yupo hai na mpenzi wake mwengine. Basi yule kaka akamwambia

Kwanini hukulazimisha ndoa kwa mtu aliyetangulia kuujua undani wako na uje kulazimisha ndoa kwangu mimi mtu nilietangulia kuzijua tamaa zako?

Rafiki zako wote uliokuja nao sike ile Yule niliekuagiza kwake alikua mstaarabu sana kati ya marafiki zako wote, hakunywa pombe, hakuupenda mziki mlimlazimisha tu kuja mara nyingi alikua ni mtu wa kukaa chini, mara kwa mara alisisitiza tirudi nyumbani. Hata tulivyokua tukiondoka alinambia ni vema na wewe uneenda kupumzika maana umechoka pia sisi nyumbani tutakwenda wenyewe sio mbali na hapa tukichukua Tax. Wote mlimbeza na kumwabiaaa ebuuuuu huko hiyo ndo kazi ya mwanaume tupeleke sie utupe na hela ya supu kesho. Hivi mlimpata wapi rafiki kama yule mbona haendani na ninyi? Yule msichana huku akilia akajibu yule ni house girl wetu huwa napenda kutoka nae ili baba na mama wasihisi nakwenda kufanya mabaya huko niendako. Basi yule kaka akamwambia nenda kamwambie house girl wenu kuwa 'Nampenda sana aje kwangu afanye kazi ya kunipenda kwa dhati nami nitamlipa upendo'.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz