AMANI YA MOYO NI MUHIMU KULIKO PENZI LA MSALITI - EDUSPORTSTZ

Latest

AMANI YA MOYO NI MUHIMU KULIKO PENZI LA MSALITI


• Kamwe usihisi kama ulimwengu ndio unakaribia mwisho pale akupendae anapokuacha.
MUACHE AENDE !
• Kujaribu kumlazimisha mtu akupende ni sawa na kujaribu kumlazimisha Nguruwe kutambua usafi na uzuri. Usimlazimishe akupende, mwache mwenyewe akupende, kama hakupendi...
MWACHE AENDE !
• Wewe ni wa thamani mno kulilia penzi. Mtu ambae anakupenda kweli atakuheshimu na hataku 'treat' kama uchafu. Kama atakuchukulia wewe kama uchafu...
MUACHE AENDE !
• Usipoteze muda wako wa thamani kujaribu kumshawishi au kuomba mapenzi. Mtu mwingine pembeni anakupenda wewe kwa dhati, ila wewe uko busy mno kumuogesha nguruwe! Kwanini?
MUACHE AENDE !
• Usikasirike pale mtu wako anapompenda mwingine tofauti na wewe. Siku zote hua ni vigumu kumshawishi NYANI kwamba Asali ni tamu kuliko ndizi...hata kaka Emanuel Msoka Admin wa Online News Tz page inayoongoza kwa makala nzuri Facebook kwa sasa Tanzania anasistiza kila siku.
MUACHE AENDE !
• Mwanamke/mwanaume yeyote anaekuchukulia kirahisi siku zote atachukulia faida kwako, atakugeuza atakavyo kama chapati akijua hufurukuti, yeye sio Mungu wa kukufanya atakavyo...
MUACHE AENDE !
• Kuna watu hawatakupenda hata kama utajitoa kiasi gani kwao. Ni sawa tu. Kukukataa kwao haimaanishi kwamba una kitu kibaya, bali ni maana kwamba hawako kwa ajili yako. Usilazimishe duara kuwa pembe tatu...
Na unaamini hukumkosea basi usiumie sana mungu yupo na ni niwakwetu sote razima tu alipe kwa alio yafuanya ata kama no lin
MUACHE AENDE !
CHA KUJIFUNZA
• Hauwezi badilisha maoni mabaya ya watu juu yako, ila unaweza ukazuia maoni yao mabaya yasikubadilishe wewe kama wewe!
• Acha kichwa chako kiongoze moyo wako kukuondoa katika mahusiano sumu. Lengo la mahusiano sio kuleta mafadhaiko ila ni kuongeza furaha juu ya ile uliyokuwa nayo mwanzoni ulipokuwa haupo ktk mahusiano.
NI NGUMU SANA ILA KWA MUSTAKABALI WA FURAHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE ME NAKWAMBIA MUACHE AENDE MPE NA NAULI KABISA!
Kama ipo ipo tu...!
Tupo pamoja??




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz