MADHARA YA MUME KUEGEMEA UPANDE WA NDUGU DHIDI YA MKEWE. - EDUSPORTSTZ

Latest

MADHARA YA MUME KUEGEMEA UPANDE WA NDUGU DHIDI YA MKEWE.

Muakilishi TZ | UTAFITI: HIZI HAPA SABABU ZA MAPENZI YA MBALI KUTODUMU
🍄🍄 _Miongoni mwa mambo yenye kusikitisha sana ni pale kitovu cha mgogoro kati ya wanandoa kinapotoka nje ya nyumba yao, pale upande mmoja wa familia zao unapoingilia maisha yao. Mara nyingi inapotokea familia ya mke ikawa haina utaratibu wa kuingilia mambo ya binti yao kwa hofu ya kuyumbisha nyumba yake, basi utakuta familia ya mume inakuwa sehemu ya uendeshaji wa maisha ya ndoa ya mwanao aliyeoa. Mara nyingi jambo hili husababisha matatizo yanayotokana na mke kutoridhishwa na uingiliaji kati wa wazazi wa mume ndani ya maisha ya ndoa yao. Hufikia hatua mke akahisi kuwa mama mkwe anachukua mamlaka yake katika kupangilia na kuendesha familia...._
🍄🍄 _Inajulikana wazi kuwa mara nyingi mama wa mume hupenda kuingilia maswala ya maisha ya ndoa na ya kifamilia ya mtoto wake kwa imani kwamba anamlinda dhidi ya harakati na mipango ya mke. Na mara nyingi mume anapokuwa hana mtazamo wa mbali hujikuta akishawishika na hatua za mama yake na kuona kuwa msimamo wake ni sahihi licha ya kwamba msimamo wa mama yake unakuwa na lengo la kumfanya awe na shaka dhidi ya mkewe kwa kuamini kuwa lengo la mama ni zuri kabisa. Hapo huwa anaipeleka ndoa yake katika shimo la matatizo na migogoro._
🍄🍄 _Mume makini na mwerevu anayetaka mahusiano yake na mkewe yawe salama, atauchukua ushauri wa mama yake, lakini hatoueleza mbele ya mkewe ambaye akijua kwamba mama mkwe anaingia maisha yake ya ndoa atachukua hatua za kukabiliana na mume kwanza kisha kukabiliana na mama mkwe. Hapo mambo huchukua mkondo mpya ikiwa ni pamoja na kutuhumiana na kuifanya ndoa kujaa migogoro, magomvi na chuki kati ya familia za mke na mume. Mume kuegemea upande wa ndugu zake dhidi ya mkewe ni rahisi iwapo hatokuwa namkini na kuchunga misingi ambayo inamuunganisha mke na mama mkwe...._
🎯💠🎯💠🎯💠🎯💠🎯💠🎯
🍄🍄 _Iwapo hatochukua hatua hiyo, akapendelea kuegemea upande wa wazazi wake wenye msimamo hasi dhidi ya mkewe, hapo mke atagundua haraka sana na kuchukua hatua za kujihami, jambo ambalo litamfanya awe na chuki dhidi ya wake zake, hali ambayo itaibua mgogoro na ugomvi. Hali itakuwa mbaya zaidi iwapo mume hatokuwa makini akaenda kuwaambia ndugu zake kila linalotokea kati yake na mkewe, jambo litakalofanya familia za pande mbili kuibuka na kila moja kuuhami upande wa mtoto wao...._
🍄🍄 _Mtu wa kwanza kabisa anayetakiwa kuchukua hatua maridhawa za kuepusha mgongano kati ya mke na mama mkwe ni mume mwenyewe. Mume anatakiwa kutengeneza mapenzi mazuri kati ya mkewe na mama mkwe na kuwafanya wapendani..
_
🎯💠🎯💠🎯💠🎯💠🎯💠🎯
🍄🍄 _Mume anatakiwa kutambua kuwa mahusiano kati ya mke na mume anatakiwa kujengwa kwenye upendo, utulivu, huruma na mahabba...._
🍄🍄_Kwa upande mwingine, mke akiona mume anaegemea upande wa ndugu pindi inapojitokeza migogoro kadhaa wa kadhaa, ajue *NAMNA* ya kushughulikia hali hii kwa subira, hekma na upole, kwa sababu siku zote subira ina malipo. Na pia mke anatakiwa kujua kuwa miongoni mwa haki za mumewe juu yake ni kuwakirimu wazazi wake na kuamiliana nao vizuri, huku akifanya subira juu ya muamala wowote usiokuwa wa kawaida unaoweza kutoka kwa wakwe zake, kwa sabababu siku zote moto huwezi kuuzima kwa moto, bali huzimwa kwa maji...._
🍄🍄Naye mume anatakuwa kuzishinda hisia za umimi na kujizuia kuegemea upande wa nduguze dhidi ya mkewe… pia anatakiwa kuwa makini anapoletewa habari fulani fulani… sio kila habari ina ukweli, kuna habari nyingi za uongo. Chukua tahadhari...
🍄🍄 *Mwisho*🍄🍄
Wanawake na ndoa zetu
💙💙💙💙💙💙💙💙💙💙
🎯🎯🎯🎯🎯🎯🎯🎯🎯🎯 by brayton🔞🔝🌟
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz