IVI KUCHEPUKA NI UJANJA AU UBOYA - EDUSPORTSTZ

Latest

IVI KUCHEPUKA NI UJANJA AU UBOYA

Wanawake wanapenda mapenzi ya gizani - Mwananchi
Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa Obssesed na Wedding Ceremony Imaginations, bila kujua Ndoa inaenda mbali zaidi!
Kuna Ndoa na kuna Harusi...Wengi mnapenda zaidi harusi, na mnapowaza Ndoa picha inayowajia ni Suti kali, Boonge la Shela kutoka Uturuki, Make Up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni, Mashosti kuingia ukumbini na Wimbo wa Alingo,Wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokuwa kali pale Karimjee Hall.. Je, umewahi kuwaza Mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia?? Umewahi kuwaza Watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?? Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno ya Mama Mkwe na Mawifi kwamba unawajazia Choo cha kaka yao na huna kizazi?? Ndoa ni zaidi ya Sherehe ya Harusi. Baada ya yale Matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni Majukumu mazito na Kiapo kisichovunjika. Achana na Fantasy za Kwaito,waza mbali kidoogo... Je, Uko tayari kuwa Mme au Mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex watarejea kidogo kidogo kama hupati Satisfaction ya kutosha kama ya Ex wako??? Huwa mnawaza hayo au mnawaza Zawadi ya Kamati itatoa Verossa ya kuanzia maisha?? Sidhani... Kabla ya kuoa na kuolewa jiulize,Unatamani Ndoa au ni tamaa ya Sherehe ya Harusi????-
Salute to the composer of this article...please SHARE
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz