```Leo hii utacheza na hisia za mtu bila wasiwasi ukidhani unamkomoa na kibaya zaidi unafurahia maumivu yake. Unamsaliti na kumdharau huku ukimshusha thamani na baadae unamuacha au yeye mwenyewe anaamua kukubali yaishe na anaachana nawe.
Mwisho wa siku nawe unaanza kuvurugwa na mahusiano yako hadi unaanza kujutia na kujiuliza ni malipo ya machozi uliyomtoa mwenza wako aliyepita au laana! Hupati majibu na unaendelea kubaki njia panda kila iitwapo leo na maisha yako ya mahusiano yanakua ya kutangatanga tuu bila mwelekeo wala mwanga maishani.
Ndugu, jifunze kuheshimu hisia za mtu na utu wake ili nawe ujiepushie na maumivu na majanga yanayoweza kutokea huko uendako.🖐🏻```
No comments:
Post a Comment