LAZIMA TUKUBALIANE KWAMBA TUNAPENDANA TU KWA SABABU YA HADHI ZETU - EDUSPORTSTZ

Latest

LAZIMA TUKUBALIANE KWAMBA TUNAPENDANA TU KWA SABABU YA HADHI ZETU


MAPENZI – Page 52 – My Blog
Katika maisha nilazima tukubaliane na ukweli kuwa tunapendana kutokana na hadhi zetu. Hilo ni jambo ambalo mara nyingi tunajidanganya kuwa mepenzi hayachagui ila mara nyingi huchagua, ingawa kuna wakati haya mambo hayaangalii ila mara nyingi watu tunaowatongoza na watu wanaotukubali ni wale ambao tunawamudu na su vinginevyo.
Mfano ningekua na hela mimi mngesikia ndiyo Jay-Z namiliki kitu cha Beyonce lakini najua si hadhi yangu. Lakini tuache huko, hata katika maisha ya kawaida kuna watu unaona kuwa huyu nikimtongoza naweza kummudu, kwamba hata akikukubali angalau unaweza kumtoa out yaani ni wa hadhi yako naamini mnanipata, ukubali ukatae ujue kuna hadhi.
Sasa wakati mwingi watu wanakukubali kwakua mnafanana, lakini kama mmoja hadhi yake ikibadilika unakuta wanatafuta watu wa hadhi nyingine. Unakuta mwanaume alikua na mwanamke wa aina flani kapata pesa kidogo anamuacha anaoa mwingine, mwanamke alikua kapauka kakukubali ameng’aa anakuambia si wa hadhi yangu.
Hili swala lipo pia katika elimu, wewe ni darasa la saba au kidato cha nne, umepata mpenzi ni mwanafunzi umeamua kumsomesha. Aisee huyu akimaliza chuo akakutana na wala Boom wenzako kama akirudi kwako basi alikupenda. Huo ndiyo ukweli na kama unasomesha sasa hivi nikuambie ndugu yangu kama ni mwanamke au mwanaume jua unampandisha hadhi anakua msomi atataka wasomi wenzake.
Najua wengine mtabisha lakini ukiangalia katika kumi waliosomesha, nane wamelizwa hivyo wewe endelea kusomesha labda utakua kati ya hao wawili. Hapa ishu sio kama mtu anabadilika, hapana mwanzoni alikukubali kwakua wewe ni wa hadhi flani, alikua hajakutana na ulimwengu mwingine, akakutana na wanaume wengine umempeleka huko unategemea nini?
Hapa naomba mnielewe, usije ukasema nimesema labda msomi hawezi kuoana na mtu ambaye si msomi. Hapana wanaweza na ndoa ikawa ya furaha kabisa, lakini hii itokee kwamba msomi, tayari kashakua msomi na elimu yake kaja kukupenda wewe ambaye si msomi basi jua kua amekupenda kwani tayari alishawaona hao wengine hakuwapenda akakuchagua wewe.
Kwamba pamoja na elimu yako ndogo lakini amekuona wewe ni wa hadhi yake au kahisi atakubadilisha utakua wa hadhi yake. Lakini kama mlipendana wote si wasomi, ukampeleka shule halafu usitegemee arudi, labda kama nayeye hana bahati ya kupata mwingine au alikua anakupenda sana. Ila kama ni huu upendo wa njoo tuvumiliane hatakuacha.
Kosa si lake, kosa ni lako uliyempandisha hadhi halafu unataka aendelee kuwa na wewe. Najua kuna watu watakasirika, kuna watu wanasomeshwa watasema si kweli, kuna watu wanasomesha wataanza kuwa na mashaka, lakini hayo ni maoni yangu, wewe malizia tu ada akirudi sawa asiporudi basi utakua umetoa sadaka fungu la kumi.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz