DADA ZANGU NAOMBA NIWAPE ANGALIZO KUHUSU HAYO MAHUSIANO YAKO. - EDUSPORTSTZ

Latest

DADA ZANGU NAOMBA NIWAPE ANGALIZO KUHUSU HAYO MAHUSIANO YAKO.

mgangakazini Instagram posts (photos and videos) - Picuki.com

Wanawake wengi wanaopendwa huishi wakiamini kua wanaume wao ni tofauti na hawatabaidlika, ni jambo zuri kuishi kwa furaha bila kuwaza kuumizwa huko mbeleni, huna haja ya kuwaza maumivu ambayo hata hayapo. Lakini ukweli unabaki kuwa wanawake wengi wanaolia leo kuumizwa, kutelekezewa watoto, kuachwa wakati washatambulishwa na mengine mengi kuna wakati walikua wakipendwa na walikua hawaamini kua wanaweza kuachwa.
Kwa maana hiyo nikuwa, ingawa hutakiwi kuishi kwa hofu lakini utakua ni ujinga kuacha kujipanga na kuwaza hivi likitokea hili nitafanya nini? Ni ujinga kudhani kuwa mwanaume wako ni watofauti kaumbwa na udongo mwingine hatabadilika! Sisemi wanaume ni wakatili, hapana lakini kuna wakati mwingine watu tu huchokana hata bila sababu. Hata wanawake ni mara nyingi tu huwachoka wanaume na kutamani kuwabadilisha.
Tofauti nikuwa mwanamke akimchoka wmanaume huvumilia na kufa na la rohoni lakini wanaume wengi wakimchoka mwanamke, huchepuka na hata kumtelekeza! Mwanaume akikuchoka akakuchoka, hakuna kiwango cha uvumilivu ambachomkitamfanya kubadilika, sisei hatabadilika, hapana, anaweza kubadilika lakini si kwasababu unavumilia bali kwa sababu nyingine nyingi, labda kaishiwa pesa, nguvu za kiume zimepungua, kuna kitu kakutana nacho huko wakati anachepuka, kaambukizwa magonjwa, kanusurika magonjwa au kachoka tu kufanya ujinga na kaamua kubadilika.
Ninachotaka kusema hapa dada zangu nikuwa, wakati unafurahia mahusiano yako, ndoa na kila kitu kingine ni wakati wa kuwaza kesho yako. Waza kesho ambayo inakuhusu wewe tu, kwamba asipokuepo huyu mwanaume nitakua na nyumba yangu, kazi yangu, biahara yangu, nitakua na hiki na kile changu. Acha kwenda kichwa kichwa wewe sio spesho kihivyo na wala huyo mwanaume wako hana umalaika wowote, kuvumilia kunakufanya wewe ubaki lakini hakumfanyi yeye abaki, anaweza kukuacha na uvumilivu wako, amka na jipange kwa kesho yako.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz