KAMA MWANAUME WAKO ANAKUFANYIA HIVI BASI JUA SI MAPENZI BALI ANAKUKATA MIGUU ILI AKUBEBE UHISI UNAPENDWA! - EDUSPORTSTZ

Latest

KAMA MWANAUME WAKO ANAKUFANYIA HIVI BASI JUA SI MAPENZI BALI ANAKUKATA MIGUU ILI AKUBEBE UHISI UNAPENDWA!

Taarifa News on Twitter: "Mimi ndo Mwanamke mzuri katika Bongo ...
“Mume wangu ananipenda, ananipa kila kitu, sina haja ya kufanya kazi! Hataki nifanye biashara kwani yeye ana biashara kubwa kubwa ameniambia nisubuiri anipe mtaji hii biashara ya Icecream anasema inamdhalilishaza! Hataki nifanye kazi kwani mshahara ni mdogo, mwenyewe nimeona nibora nibaki kulea wanangu kwani walikua wananilipa hela ambayo mume wangu anaweza kunipa! Kila kitu ninachotaka kukifanya anakataa, anasema hajashindwa kunilisha, kweli nikimuomba pesa ananipa!”
Ushawahi kumsikia mwanamke anaongea hivyo, ukamsikiliza na kumuonea wivu, unakuta anaendesha gari zuri na kweli mume wake anampa kila kitu, ukatamani angalau na wewe ungekua na mwanaume kama huyo? Lakini inawezekana wewe ndiyo huyo mwanamke, mume wako hataki ufanye kazi na kila kitu unachoojaribu kukifanya anakukatisha tamaa. Maneno yake ni kama “Mshahara mdogo…hiyo kazi inadhalilisha…sijashindwa kukuhudumia…mke wangu hawezi kuajiriwa!”
Najua unadhani ni upendo, na kakua anakupa kila kitu kweli basi utakaa nyumbani na kufurahia, utajiambia “Nimeshamuambia kuhusu ajira hataki/ kila nikitafuta kazi ananiharibia/ hataki kabisa nitoke ndani…” Umeridhika na hiyo hali na unatamba kabisa kuwa unapendwa. Ndugu yangu hakuna upendo hapo, ukiona mwanaume anakufanyia hivyo si kwamba anakupenda sana labda anakuonea wivu hapana! Mwanaume anayekupenda atataka kukusapoti, kukuacha ukue na kutaka mafanikio yako!
Lakini mwanaume ambaye anataka kukucontrol kila siku atataka uwe chini yake, uwe unamtegemea, uwe unamuomba kila kitu. Mama yako akiumwa ukamlilie, ukitaka Wanja ukamlilie, ukitaka Pedi ukamlilie na kila kitu usiweze kufanya bila yeye. Unapokua hivyo anajua kuwa hata akikunyanyasa vipi, hata akikupiga vipi, hata akikutukania Mama yako basi hutaondoka kwakua huwezi kuishi bila yeye. Anajua kwamba hata ukichoka, ukataka kuondoka na akakuachia watoto hutaondoka!
Kwamba hatakua na haja ya kukuambia ondoka niachie wanangu kwani anajua ukiondoka unarudi kwenu kuwa mzigo na kama kweli nako hawakautaki au hawawezi kukuhudumia basi hutaondoka kwani huna hata hela ya kupanga. Anajua kuwa hutamaliza wiki bila kurudi kwake kuomba hela ya kula hivyo hicho unachodhani ni mapenzi jua nikuwa anakupa ulemavu. Kwamba anakukata miguu ili akubebe na wewe useme ananipenda ndiyo maana hataki nitembee kumbe kahsakufanya mlemavu.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz