BARUA KWA EX. (EX BOYFRIEND/GIRLFRIEND) - EDUSPORTSTZ

Latest

BARUA KWA EX. (EX BOYFRIEND/GIRLFRIEND)

Naitwa Angela, Naomba Muda wako japo kidogo usome stori hii mpaka ...
Dear Ex,
Siandiki barua hii kukutukana au kukukejeli. Hapana, hii ni asante yangu kwako kwa kuniacha.
Leo nimepita sehemu ambayo mimi na wewe tulikua tukienda mara kwa mara wakati tukiwa ktk mahusiano na pamenikumbusha mbali sana.
Sio kwamba nimekumiss, hapana nimekufikiria na kukufananisha na huyu niliefunga nae ndoa. Na kwa hilo nimegundua kwanini mimi na wewe tuliachana.
Nimekumbuka namna mimi na wewe tulivyokua tunagombana mara kwa mara, ni mara chache sana tulikuwa na amani ktk mahusiano yetu; Lakini kwa huyu niliyenae sasa hivi nina amani zote, hata tunapokwaruzana hua tunasuluhisha na kuwa na amani tena. Ni raha sana kuwa na amani ya moyo.
Nakumbuka namna nilivyokua nakuuliza mara kwa mara ni nini mustakabali wa mahusiano yetu yaliyodumu muda mrefu, na namna ulivyokua ukilikwepa hilo suala na kutotaka kuzungumzia future yoyote na mimi.
Lakini na huyu nilienae sasa hivi amenipa na ninao uhakika na maisha yangu. Amenipa uhuru na ninaweza kukiri kuwa ni kweli nimependwa!
Nakumbuka namna ulivyokua unanifanya nijisikie mtu niliyefeli, mtu nisiye na faida wala thamani yoyote. Nilikua nikikueleza ndoto na maono yangu lakini wala hukunitilia maanani. Lakini mpenzi nilienae hivi sasa anaamini ktk ndoto zangu kuliko hata navyoziamini mimi mwenyewe.
Nakumbuka namna nilivyojitahidi kuwa romantic kwako ili tu niweze ku-win upendo wako kwangu. Nilifanya mambo mengi sana mengine nje ya hiari yangu lakini hukulitambua hilo.
Nilichoambulia ilikuwa ni maumivu yasiyokwisha. Ila kwa huyu nilienae sasa hivi mapenzi yanakuja automatic, situmii nguvu nyingi we get well together and it's effortless.
Ulivyoniacha, niliumia sana kwa sababu kipindi kile ndicho nilikua nimekupenda na kukuhitaji sana. Nilipigwa upofu wa penzi lako kiasi ya kutokujua makusudi ya Mungu ya kunitenganisha na wewe ili nikutane na huyu niliyenae anaenistahili.
Wewe ndie niliyekujua na kujijengea matumaini ya kuja kuishi pamoja, kumbe Mungu nae alinijua zaidi na akanitenganisha na wewe ili nije nikutane na huyu anayenistahili. Sasa nimeamini muda mwingine Mungu hutuondoa makusudi pale ambapo hatustahili bila kujalisha ni namna gani tutaumia.
Nilihangaika mno kukupenda pasina kujua haukua fungu langu. Nilishakusamehe kwa namna ulivyoniumiza mara kwa mara na bila shaka hata wewe ulinisamehe kwa pale nilipokukosea.
Nakuombea kama una wazo la ndoa, basi upate mtu ambae ataendana na wewe na kukupenda vile utakavyompenda. Ila kama huna wazo hilo ni bora ukaanza kuliweka akilini maana hua kuna point of no return na neno NINGEJUA huja mwisho wa safari.
Sometimes sio kwamba watu hawajui kupenda au hawataki kupenda, bali ni kwa sababu watu walionao au waliokua nao, hawajui kupokea na kuheshimu upendo wanaopewa. Kama mimi tu, nilipenda kweli sehemu ambayo sikupendwa. Ila atleast sasa nimepata mahala pa kupenda nilipopendwa. NIKIKUMBUKA ULIVONITENDA MACHOZI YANITOKA
Nakutakia kila la kheri.
Asante sana kwa kuniacha,
Your EX
SIGNED
"No matter how hard your heart is broken, the world doesn't stop for your grief "
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz