Hivi yuko wapi mwanawake mwenye sifa hizi: ______👇🏾______ - EDUSPORTSTZ

Latest

Hivi yuko wapi mwanawake mwenye sifa hizi: ______👇🏾______


Mwanamke anayeona uko katika hali ngumu ya maisha kiuchumi, hauna hela, badala ya kukuacha, anasema "usihofu mme wangu", anakutia moyo kuwa "usijali siku moja nasi tutapata, sijakupendea pesa", pesa ni makaratasi tu, penzi ni kipaumbele". Kisha anashirikiana nawe bega kwa bega kutafuta maisha.
__-__-__
Mwanamke yule anaelia sababu anakupenda au kukukumbuka. Mwanamke ambae akisikia unaumwa, yeye anaumwa mara mbili zaidi yako, si kwamba anaigiza, bali kwa vile anaona mwili wako kama uko ndani ya mwili wake mwenyewe.
___💞___
Mwanamke asiyekubali kukupoteza, anaejaribu kukurudisha wakati mmekwazana. Alie tayari kusamehe hatakama ni yeye ndo kakosewa, yu radhi kusamehe ili tu asikupoteze
_-_-_
Mwanamke ambaye hata umuumize kiasi gani, bado atakuambia anakupenda na yu radhi kukufanyia yote utakayo; kwani anakuhesabu wewe kuwa ndo furaha yake kamili.
_(🌹)_
Mwanamke anaeacha kurumbana na wewe ili kuunusuru uhusiano wenu; anaefanya ujisikie wewe ni wa pekee kwake; na kujaribu kukupa furaha
~~~
Mwanamke anaetoa tabasamu lake halisi kila akuonapo au kusikia sauti yako tu.
------
Mwanamke anaetaka kukuacha sababu ya ukorofi au tabia nyingine zinazomkera, lakini hakuachi; anaesema anakupenda au kukumbatia mbele za watu bila kujali macho yao.
*****
Mwanamke alie mwaminifu kwako kupita maelezo; anayesimama imara kukilinda penzi, mwanamke ambae wengine walimfuata anawatolea nje na kuwaambia ukweli kuwa tayari nina mtu.
Mwanamke anaekuwa karibu na wewe zaidi wakati wa matatizo.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz