💞 *FAIDA ZA KUMKUM-BATIA MKEO/MUMEO MKIWA KITANDANI* 💞 - EDUSPORTSTZ

Latest

💞 *FAIDA ZA KUMKUM-BATIA MKEO/MUMEO MKIWA KITANDANI* 💞

Hizi ndio faida za kumkumbatia mumeo/mkeo – Usiku wa Mahaba
Umewahi kufikiria faida zinazopatikana kwa kumkumbatia mkeo/mumeo mkiwa mmelala? Famasia yako ya Furaha ya Ndoa inakuletea faida 6 za kukumbatiana kitandani:
1⃣ *HUPUNGUZA SHINIKIZO LA KISAIKOLOJIA:*
Unapomkumbatia mkeo/mumeo mkiwa mmelala husaidia kuzalisha kichocheo (homoni) cha furaha kiitwacho oxytocin. Homoni hii hufanya kazi ya kupunguza hatari ya kupatwa na maradhi ya moyo na kupunguza shinikizo la kisaikolojia. Hilo pia hupelekea kupunguza hatari ya kupatwa na maumivu ya kichwa na maradhi mengine.
2⃣ *USINGIZI MARIDHAWA:*
Wanandoa wanapokumbatiana husaidia kulala vizuri. Tafiti mpya zimeonesha kuwa kumbatio hupunguza cortisol na hivyo kupunguza shinikizo la kisaikolojia. Pindi cortisol inapopungua mwilini, moja kwa moja usingizi huwa mzuri na mwanana.
3⃣ Unapomkumbatia inaweza kusababisha raha, hasa mambo yanapofikia kwenye hatua ya kucheza, lakini kabla ya hapo furahia ladha ya mgusano wa ngozi zenu kabla ya kusonga mbele… Moyo wako unatakiwa kuuhudhurisha katika eneo na muda wa mgusano huo ili kujenga uaminifu na hisia za ushirika.
4⃣ *KUKUMBATIANA HUWAPA FURSA YA KUWASILIANA BILA KUONGEA*.
Na hili ni jambo maridhawa kabisa kwa wanandoa kuzidi kuwa karibu.
5⃣ *NI DAWA YA FADHAA:*
Kimbilia kitandani. Kumbuka kuwa kitanda kipo kwa ajili hiyo. Achana na kitabu, televisheni, simu, tablet na mambo mengine kama hayo. Kumbatio litakusaidia kumakinika na kupata utuvu.
6⃣ *HUWAPA HISIA ZA KURIDHIANA NA KUTOSHEKA:*
Mnapokumbatiana bila kuwa na lengo la kuingia kwenye tendo la ndoa, mtapata hisia kubwa ya kuridhika na ndoa yenu. Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa wanandoa wanaokumbatiana wanaridhika sana na ndoa zao kuliko wale wasiokumbatiana.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz