DEAR LADIES, NAOMBA MUYAJUE HAYA - EDUSPORTSTZ

Latest

DEAR LADIES, NAOMBA MUYAJUE HAYA


👉Usifichue udhaifu wa mumeo kwa familia na marafiki zako. Itakurudia. Wewe ni mlinzi wa mumeo, naye ni mlinzi wako pia.
👉Usitumie mihemko yako hasi kuwasiliana na mumeo, hujui namna mumeo atakavyoitafsiri. Wanawake wenye hulka ya kujihami huwatengenezi nyumba yenye furaha.
👉Usimlinganishe mumeo na wanaume wengine, hujui maisha yao halisi yalivyo. Ukiibomoa hadhi yake, upendo wake kwako utashuka.
👉Usisahau kuwa mumeo alikuoa, yeye si mfanyakazi wako au mtu mwingine tofauti. Tekeleza majukumu yako.
👉Usimpe mtu mwingine fursa ya kumhudumia mumeo, watu wanawaweza kufanya mambo mengine, lakini huduma za mumeo ni jukumu lako mke.
👉Usimlaumu mumeo akija nyumbani mikono mitupu. Badala yake mpe nguvu, mhamasishe na kumshajiisha.
👉Usiwe mke mwenye matumizi ya hovyo, jasho la mumeo halitakiwi kutumiwa hovyo.
👉Usijifanye kuwa mgonjwa kwa lengo la kumnyima tendo la ndoa. Mpe kwa namna apendavyo. Tendo la ndoa ni muhimu sana kwa wanaume, ukiendelea kumnyima haitachukua muda mrefu kabla mwanamke mwingine hajatimiza jukumu hilo. Hakuna mwanaume anayeweza kustahmili kukosa tendo la ndoa kwa muda mrefu.
👉Usimlinganishe mumeo na mwanaume wako wa zamani kitandani. Ukifanya hivyo, nyumba yako inaweza kupata mtikisiko wa aina yake.
👉 Usijibishane na mumeo hadharani. Hilo litashusha hadhi na heshima yake. Hitajio namba moja la mwanaume ni heshima.
👉 Usimpe changamoto mumeo mbele ya watoto. Wanawake wenye busara hawafanyi hivyo.
👉 Usisahau kumuandaa mumeo na kuhakikisha kuwa yuko maridadi kabla hajatoka nyumbani.
👉 Usiruhusu marafiki zako kuwa karibu mno na mumeo.
👉 Usiwe na haraka unapokuwa bafuni na kwenye dressing table. Huko nje mumeo anakutana na wanawake ambao wanatumia muda wao kujiremba vizuri bila haraka yoyote ili waonekane maridadi.
👉 Wazazi au familia yako hawana uamuzi wa mwisho katika ndoa yenu. Endelea kuwaheshimu, lakini wasiwe na uamuzi wa mwisho kuhusu ndoa yenu.
👉 Usiegemeze upendo wako kwenye vitu vya pesa. Endelea kumheshimu mumeo licha ya kwamba unapata pesa zaidi yake.
👉 Usisahau kuwa mume anahitaji mtu anayemakinika naye na kumsikiliza vizuri, hivyo unapozungumza naye acha mambo mengine. Mawasiliano mazuri ndiyo msingi wa nyumba yenye furaha.
👉 Mke mvivu hajali. Hata hajui kwamba anatakiwa kuoga na kuwa msafi.
👉 Je, mumeo anapenda chakula fulani? Kuwa makini sana kwenye namna ya utayarishaji wa chakula. Hakuna mume anayefanya maskhara na suala la chakula.
👉 Usiwe mtu wa kumkamua sana mumeo, ukataka kila kitu uwe nacho wewe. Furahia kile kinachopatikana kulingana na uwezo wake.
👉 Ifanye glasi ya maji kuwa ukaribisho wa kwanza kwa mumeo na kwa kila mgeni anayeingia nyumbani kwenu. Ukarimu maridhawa ndiyo uzuri wa kweli.
👉 Ndoa yako itakuwa na thamani kama utaipa thamani. Uzembe na kutojali ni sumu ya ndoa.
👉 Watoto ni zawadi adhimu kutoka kwa Mungu, wapende na uwafunze mambo mazuri.
👉 Mke anayemuabudu Mungu ni mke maridadi, daima muombee mumeo na familia yako.
Ili kujifunza zaidi namna ya kutunza au kuimarisha Ndoa, Uchumba/Mahusiano yako, ungana nasi katila group letu la whatsApp "ITUNZE NDOA YAKO" kwa kunitumia ujumbe wako kwenye whatsApp inbox yangu kwa nambari 0717 442 212.
Au bonyeza link hapo chini ikupeleke moja kwa moja kwenye whatsApp inbox yangu
👇👇👇
Share
Like Page




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz