DADA ZANGU NAOMBA IWAAMBIE JAMBO HILI KUHUSU WANAUME - EDUSPORTSTZ

Latest

DADA ZANGU NAOMBA IWAAMBIE JAMBO HILI KUHUSU WANAUME

FAHAMU JINSI YA KUISHI NA MPENZI ANAYEPENDA FEDHA - Lemutuz Blog

DADA ZANGU siju hata kwanini hamuelewagi, hivi unapokuta meseji za mwanamke mwingine wkenye simu ya mume wako, unaposikia huko mtaani kuwa mume wako anatembea na flani, unapokuja kumuuliza mume wako unakua unataka nini? Yaani hivi ninavyowaambia kuwa ukifumaniwa kataa unafikiri ni maneno yangu?
Nakua nawafundisha tu namna akili za mwanaume zinavyofanya kazi, kwamba mwanaume hata ukimfumania anafanya mapenzi hapo na mwanamke tena chumbani kwenu unaona kabis aile ingia toka ingia toka atakataa, atakuambia si yeye yaani anaweza kukataa kabisa na kukuambia hajui kilichotokea.
“Nimeshangaa tu nimekuja na huyu mwanamke humu ndani, sijui kaniwekea dawa au ni nini lakini mke wangu hizi nina uhakika si akili zangu, hivi kweli hata kama mimi ni Malaya kiasi gani ningekua mjinga mpaka kumleta mwanamke wangu humu, fikiria mke wangu, kuna mtu anatuchezea, hii ni kazi ya shetani, tuombe, tufunge kuna mtu anachezea ndoa yetu!”
Anaongea mpaka unaamini, hapo umemfumania umeona kwa macho yako, sembuse wewe eti umeona Concom imetumika, sijui picha za uchi, sijui vimeseji unampeekea mwanaume Baharia kabisa unataka akubali! Dada zangu kanuni ya mwanaume ni Kataa! Kataa! Kataa! Sasa unapojikusanyia maushahidi yako huko kaa nayo, ukimfuata mwanaume kuwa akubali unapoteza muda tu! Kaa nayo kama unamuacha muache kama unabaki baki!
Unaponifuata na mimi na kuniambia nimemfumania mwanaume wangu akakataa siriasi unaniboa, natamani hata nikukatie simu maana ni kama hunisomi. Ishu iko hivi, ukiona mwanaume kakubali basi jua kashakusoma kuwa huondoki, ashakusoma kuwa hata akikubali haina madhara, lakini pia ukiona kakubali jua kuwa hajali, uondoke usiondoke kashachoka nayeye.
Achene kuuliza uliza eti unatembea akubali kwani yeye ni mjinga! Na vitu vingine mnauliza mpaka mnaboa, hivi unaona katumiwa picha za uchi bado unauliza, ulidhani aliyemtumia ni Mama yake au Dada yake, kwamba familia yao inapendana sana mpaka inatumiana picha za uchi, umeona ni kweli amua mwenyewe acha kusumbua watu, ulizichokonoa mwenyewe ya nini unamuuliza uliza!

Image may contain: one or more people, people sitting and indoor




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz