ANAKUTAKA KWAKUA NI RAHISI KUTEMBEA NA X KULIKO KUTONGOZA MWANAMKE MPYA! - EDUSPORTSTZ

Latest

ANAKUTAKA KWAKUA NI RAHISI KUTEMBEA NA X KULIKO KUTONGOZA MWANAMKE MPYA!


Karibu kila mwanaume akikutana na kila X wake kuna kitu kimoja ambacho atakikumbushia, inawezekana ikawa ni chakweli au hata kingine ni cha uongo lakini wanaume wanafahamu kua ni rahisi kumdanganya na kumpata tena X wako kwa kumuambia kila wakati unakumbuka kitu flani ambacho kwa mke/mpenzi wako hukipati. Hiyo ni tabia ya karibu kila mwanaume ambaye ana X, wale ambao hamna ma X poleni.
Kwa bahati mbaya nikua kama mwanaume ni muongeaji mzuri basi wanawake nao huamini kua labda nikweli jamaa kammiss, tena kama mwanaume ndiyo alimuacha mwanamke, tena labda kwa mbwembwe, akimuambia “Daaa najuta hata kwanini tuliachana, sijakutana na mwanamke kama wewe, yaani jinsi ulivyokua unananihii mpaka sasa hivi nikiwa na mke wangu navutia picha ile nanihii yako ndiyo namaliza kunanihii!”
Hapa mwanamke hufurahia kwani anaona kua kumbe mimi nilikua balaa lakini kumbe pamoja na kuniacha lakini bado hajamove on. Labda nikuambie tu dada yangu hajakukumbuka chochote, tena inawezeka mpaka mnaonana alikua hakumbuki hata jina lako vizuri, hicho kitu kakikumbukia hapohapo na mbaya zaidi hatakikumbuka tena mpaka akuone tena siku nyingine.
Tena kuna wale wanaume ambao labda yuko Dar na wewe uko Mwanza, kila akitaka kuja Mwanza ataanza kukutafuta mapema na kukumbulisha namna ambavyo ameshindwa kukusahau, tena wakati mwingine anakupigia simu usiku mpaka unamuulzia, mkeo yuko wapi huogopi kukamatwa anakujibu “Hata sijali huyu akishalala kama kameza dawa ya usingizi!” Anampondaponda na wewe unajisikia rahaa na kujiona spesho halafu unamsikia “Nataka nije Mwanza, inabidi safari hii tuonane!”
Kwa bahati mbaya dada zangu mnasisimkwa sana, mnatuamini ila nikuambie tu kama unajipenda, unajithamni na kama uko kwenye ndoa au mahusiano yanyoeleweka mblock huyo mtu. Narudia mblock huyo mtu kwani hata hajakukumbuka! Mwanaume kama alikuacha akikukumbuka anakufuata na si kusubiri miaka eti anataka kuja ulipo au anakuona bahati mbaya anakuambia nimekukumbuka! Hapo anawaza “Huyu fala nigonge kirahisi nisepe!” Anakutaka kwakua ni rahisi kutembea na X kuliko kutongoza mwanamke mpya! Wala huna jipya usijishaue!
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz