ACHA NIKUAMBIE KITU!! - EDUSPORTSTZ

Latest

ACHA NIKUAMBIE KITU!!


ni mambo 10 tu muhimu na ya kuzingatia ๐Ÿค”.
***************** ******************** × *********
1.=>Ukimhukumu samaki kwa kushindwa kupanda mti utakua umekosea, wewe mtupie kwenye maji uone atakavyo kata mawimbi. Kuna mahali ukiwekwa utafanya vitu vya ajabu mpaka Dunia itashangaa.๐Ÿ˜‰
2.=>Usimpotezee mtu anayejitahidi kukujali. Siku akiondoka ndio utagundua ulikua bize unaokota mawe badala ya dhahabu.๐Ÿ˜˜
3=>Kwa nini unahangaika na kuumia unaposemwa vibaya na watu wasio kufahamu kiundani? Inamaana hujui kuwa mbwa hum'bwekea mtu asiyemfahamu.๐Ÿ˜‚
4.=>Unapopaka make-up ili upendeze, jitahidi pia kuupendezesha moyo wako kwa kufanya matendo mema maana haina maana kupendeza usoni wakati moyoni ni pachafu.๐Ÿ˜‰
5=>Usikimbilie kuolewa au kuoa mtu tajiri, olewa au oa mtu mwema maana hakuna tajiri atakayeweza kuununua moyo mwema na moyo mwema ni chanzo cha amani na amani ikiwepo ndo kufurahia maisha sasa.๐Ÿ™ƒ
6=>Hii na wewe chukua na weka akilini kabisa, ukitaka kupunguza matatizo katika maisha yako jitahidi uwe unafuata utaratibu.๐Ÿ˜‹
7=>Nakwambia ukweli na wewe ndio unamjua, watsap anauwezo wa kuku-block, instagram anauwezo wa kuku-block na facebook anaweza kuku-block lakini kamwe hawezi kuzi-block baraka zako kutoka kwa Bwana wa mabwana zitokako mbinguni.๐Ÿ˜
8.=>Hivi unawezaje kuuza ng'ombe wako eti tu kwa vile umepata oda ya ngozi. Ukiona mtu anachezea utu wako kaa nae mbali maana watu wengine ni kweli kama mkaa, asipokuunguza basi atakuchafua.๐Ÿคช
9.=>Hivi, ulishawahi kuona mti uko bize unasumbuka na majani yaliyoanguka? Mti hua bize kutengeneza majani mapya, nawewe kuwa bize kutengeneza na kukaribisha vitu vipya na sio vilivyopita.๐Ÿ˜œ
10.=>Swali lenye majibu ya maisha yako yote, Je hicho unachokifanya ndicho Mungu alichokuleta Duniani ukifanye? Kama jibu lako ni hapana, basi unahaki kuendelea ku-struggle bila faida?? (follow me as first)๐Ÿ˜‰
Bonus
=>Ukiona moyo wako unagoma katika jambo flani, acha, Mungu anakuepusha na balaa maana moyo una macho ya kuona mpaka mwisha sema hua tunapuuzia tu....!!
Dondosha comment yako kama umepata cha kujifunza.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz