WIVU NI KIDONDA UKISHIRIKI UTAKONDA! - EDUSPORTSTZ

Latest

WIVU NI KIDONDA UKISHIRIKI UTAKONDA!


Image may contain: 3 people, people smiling
Ilikuwa asubuhi wakati nikiosha gari la bosi wangu wa kiume Yaani Baba mwenye nyumba, Punde nilipomaliza nikaelekea jikoni ili nishirikiane na mwenzangu "HOUSE GIRL" ndipo nilipomkuta Boss wangu wa kiume akiwa amekumbatiana na Mtumishi mwenzangu, Ghafla nikawa nataka kugeuka kurudi ili wasinione lakini nimeishachelewa na nilikutanisha macho na Dada wa kazi kwa mshangao wake alisababisha boss kugunduwa kuwa Kuna mtu amewaona, Waliachiana haraka na boss akaniita na kuniuliza Nafanya nini pale nami nikamwambia nilikuja kuangalia maandalizi yako ya chai Kwani mwenzangu alikuwa anakuandalia nami nikawa naosha gari huko nje... Kwa aibu aliondoka na kutuacha jikoni wala hakusema kitu, Nilisikia wivu sana kwani Bianca alikuwa mtu wangu Kwani tuliishi banda la uani na hiyo ilitupa nafasi ya kuwa wapenzi japo tulikuwa waajiliwa wa nyumbani kwa Petro, Bianca ndo maana siku hizi nikikuita hauji kumbe unatoka na boss? Wewe nae uache wivu wako unafikiri nikimnyima atapenda? Bianca alinijibu kwa ufupi sana tena alionekana kutaka nijue kuwa wameanza siku nyingi, Sasa Bianca kama unaona umeanza kutoka na boss si ungeniambia ili Mimi nikajitoa kuliko kuniumiza hivi, Hivi wewe John Una akili kweli Naanzaje kumkataa boss? Bwana kama unaona vipi sepa tu Mimi ndo kwanza nimeahidiwa kupangishiwa na muda si mrefu nitaondoka hapa! Niliumia sana lakini nikakosa Jibu la kumpa nikabaki mpweke nisiyejuwa hatma yangu na Bianca maana tuliahidiana kuoana, John Uko wapi? Alikuwa boss akitaka kujuwa nilipo ndipo nikaitika na kutoka kumfuata huko nje, John nenda pale shekilango nichukulie bahasha yangu kuna mtu utamkuta kituo cha mafuta cha TOTAL... Sawa boss! Niliitika na kutoka kuelekea huko lakini moyoni nikiwa nimejawa wivu nikiwaza nimewaacha boss na Bianca wawili tu watakuwa wamenituma makusudi wafanye yao, Nikapanda boda boda kuelekea huko shekilango na kwa bahati nikapata mzigo wa boss na kurudi faster nikafika home na kukuta mageti yamefungwa, Simu ya Bianca inaita tu kwa muda kama dakika 20 nikasikia honi boss akimhimiza Bianca afungue geti, Geti likafunguliwa na gari likawa linatoka getini alikuwa Boss akaniuliza UMEPATA? Ndiyo Boss bahasha hii hapa, John mama akikupigia useme nilitoka mapema, Sawa boss... Roho inaniuma sana kwani Bianca macho mekundu na pia nguo alokuwa amevaa asubuhi ameivua, nikakumbuka msemo wa Waswahili "UKIONA MANYOYA UJUE AMELIWA" Simu yangu ikaita alikuwa Mama Yaani boss wa kike, Ndiyo mama nakusikia... John baba yupo? Hapana mama ndo ametoka, nilimjibu boss na nikaona kama ameshusha pumzi, Bianca yuko wapi? Yupo nyumbani mama, Na wewe ulikuwa unafanya nini? Nilikuwa nimetumwa na baba huko shekilango, John ina maana ulipokwenda shekilango ulimuacha baba nyumbani akiwa na Bianca? Ndiyo mama! John unaonaje mienendo ya Bianca na Mume wangu? Alikuwa mama Yaani Boss lady akitaka UBUYU toka kwangu, Kama ujuavyo nimewashuhudia boss akikiss na Bianca na ukumbuke kuwa Bianca ni mpenzi wangu, Bianca ameonyesha hanitaki tena, wivu nao umechukuwa nafasi kubwa hata inanipa hasira Basi nikajisemea KAMA NOMA ACHA IWE NOMA TUU... John mbona Uko Kimya? Hapana mama nilikuwa najaribu kukumbuka kama Nimeona lolote ila Mama ni kweli Bianca na baba siwaelewi maana baba akiwepo huwa ananituma wanabaki wawili tu, Asante John Naomba usimwambie mtu kama tumeongea Haya ili nilifanyie kazi, Sawa mama simwambii mtu, Nikaendelea na kazi zangu lakini tayari nimejawa Hofu ikiwa Boss wa kiume atajuwa hili, Zilipita siku Swala hilo likawa Kimya nami nimezoea kuwa Bianca hanitaki, Siku moja Boss wa kiume akaondoka na akabaki boss wa kike nae akamtuma Bianca tukabaki wawili, John... Naam mama! Njoo, sauti inatokea chumbani nami nikasogea mlangoni na kuitika tena ili boss atoke au anipe maagizo, Ingia John, kwakweli sikuogopa maana nilihisi ana kazi ambayo anataka niifanye, Nilichokiona sikuwahi kukiona tangu nizaliwe, Boss Lady aliumbika na kuwa na shape ambayo nilikuwa naiona kwenye magazeti ya sani, Nikawa nataka kugeuka ili nitoke chumbani humo ghafla nikashikwa shati na kuambiwa "KWANI WEWE JOHN MPAKA UAMBIWE UNAHITAJIKA NDO AKILI ZIKURUDIE? Hapana mama, Sasa kumbe unataka nini? Boss Lady alinivua nguo na alianza yake nami bila kuchelewa nikamparamia na ikawa kama alivyopanga yeye, Wakati wote huo najisemea moyoni PENYE MITI HAPANA WAJENZI... Boss alikuwa mwanamke haswaaa, Kwa ushamba wangu na uhaba wa wanawake siwezi kumuacha bora nife, Wakati nikiwaza hayo Bianca anagonga Mlango wa chumbani, Nasikia ila sikuitika wala boss hakuitika ndipo Bianca alifungua na kuingia Kwani alichokuwa ameagizwa ni sabuni hivyo alijuwa pengine boss Lady yupo Bafuni, Mama sabuni hizi hapa, alikuwa Bianca akimsemesha Boss Lady, Weka hapo! Bianca umetembea mara ngapi na Mume wangu? Mama huyo John muongo tuu Mimi sijafanya hivyo ila Baba alinifuata jikoni siku moja akanikumbatia ndipo John akatukuta, Na wewe leo umemkuta John umejisikiaje? Mama Mimi sina lolote ila John ni mbaya maana anataka unifukuze tu, Sikia Bianca Mimi sikufukuzi, Ila nataka nikwambie kuwa John ni Mpenzi wangu tangu leo na ninewafatilia wewe na Mume wangu nikagunduwa mna mahusiano, Na pia niliwagunduwa wewe na John mna mahusiano ila umelewa penzi la mume wangu sasa umemwacha John lakini sasa John sio House boy tena ila mpenzi wangu na wewe endelea na Mume wangu... Maneno yale yalimuumiza sana Bianca akatoka na kufunga Mlango kwa nguvu, Mimi na Boss Lady aka Honey tulitoka chumbani na kwenda kukaa sebureni, Simu ya Mama au Honey ikaita na alipopokea aliongea na mtu kama wanagombana nikagunduwa alikuwa mumewe, Walijibishana mambo mengi sana mwisho nikamsikia Boss Lady akisema "HUNIBABAISHI NITAONDOKA" Hofu ikanijaa na kujikuta namwambia Boss Lady MAMA NAONA BABA AMEAMBIWA NA BIANCA HIVYO AKIJA ATANIUA KABISAA BORA MIMI NIONDOKE KABLA HAJAJA... Hebu Acha woga, Na kama kuondoka tutaondoka Mimi na wewe, Boss Lady alikuwa akisisitiza kwa kujiamini lakini Mimi moyo umejaa hofu, Tulifungasha na kuondoka Mimi na Boss Lady huku tukimuacha Bianca nyumbani, Bianca alionekana mwingi wa mawazo lakini sikujali maana yeye ndiye chanzo, Wakati tukiondoka pale Boss Lady akapiga simu kwa mumewe na kumwambia "TUMEONDOKA MIMI NA JOHN LAKINI MKEO BIANCA TUMEMUACHIA NYUMBA MUISHI VIZURI" Wakaanza tena kutukanana na Kuna mambo aliongea Boss Lady nikajuwa kumbe hata kazi ya mume yeye ni sababu ya kuipata, Nakwambia hufiki mbali na wala sintorudi kamwe mwanaume huna aibu wala huruma utaipataje heshima? Na kwa taarifa yako John ndiye mume wangu kwanza ni mtamu kuliko wewe, MTENDA AKITENDEWA HUHISI AMEONEWA... Sikutaki tena, Alimalizia Boss Lady na tukafika katika nyumba na akaniambia KUANZIA LEO WEWE NI MUME WANGU nakuomba usiniumize, Boss Lady alimalizia nami bila hiyana nikayatoa ya moyoni mwangu HUTAJUTIA KWANI WEWE NI ZAIDI YA MAMA KWANGU! Sasa tuna watoto mapacha, Bianca na Boss wa kiume waliachana na Boss wa kiume aliisha fulia, Ujumbe huu unafundisha kuwa USIMUAMSHE ALIYE LALA UTALALA WEWE.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz