MKASA WA KUSISIMUA: MATESO YA MUME YAMENIPA MSIBA MZITO, NAJUTA UVUMILIVU UMENIPONZA. - EDUSPORTSTZ

Latest

MKASA WA KUSISIMUA: MATESO YA MUME YAMENIPA MSIBA MZITO, NAJUTA UVUMILIVU UMENIPONZA.

Image may contain: 1 person

#inasikitisha sana anasimulia GLORIA

Habari yako admin Kaka Emanuel Msoka heri ya mwaka mpya kwako na kwa familia yako nzima ya Online News Tz, kwa jina Naitwa Gloria nimeolewa ila nasikitika napitia mapito magumu mno ndani ya ndoa kiasi ambacho sasa naona nashindwa, nimechoka moyo wangu unazimika.Siku moja
Nilirudi nyumbani nikiwa nimechelewa sana na kama kawaida nilijua siku hiyo ilikuwa ni kipigo tu, kusema kweli nilikuwa nimechoka, sikuchoka kwa kipigo bali nilichoka kutokana na kazi nilizokuwa nimefanya siku hiyo. Nikisema kazi simaanishi kazi zile za ofisini, hapana, mimi si mfanyakazi, si kwamba si kusoma hapana, nina shahada yangu mfukoni ambayo niliisotea mika mingi darasani.

Baada ya kuolewa na kupata mimba nikiwa bado sijapata kazi basi niliamua kumlea mwanangu kwanza na baada ya mtoto kuwa mkubwa nilipotaka kutafuta kazi mume wangu alikataa. Kama wanaume wengi aliniuliza “Kwani unakosa nini hapa? Au unataka uende ukafanye umalaya wako huko?” Kusema kweli sikuwa nikikosa chochote kwani mume wangu ni mtu mkubwa sana serikalini.

Kwakuwa nilikuwa nikipata kila kitu basi hata sikusisitizia sana kuitafuta hiyo ajira, nilivumilia tu na Mungu akajaalia nikapata mtoto wapili na watatu. Miaka kumi na mbili kwenye ndoa sasa na tangu siku ya kwanza kuna vitu vingi vimebadilika kasoro kitu kimoja tu, kupigwa karibu kila siku ya Mungu.

Nilivumilia kupigwa mpaka kufikia hatua ya kuona kama kitu cha kawaida, nikaanza kuona kama sehemu ya majukumu ya ndoa, kupigwa. Mpaka sasa bado naona hata aibu kuvua nguo mbele za wanawake wenzangu kutokana na mistari ya mikanda, fimbo na makovu ya maumivu ya kila siku. Lakini kama walivyo wanawake wengi ambao wako kwenye hali kama yangu nilikuwa navumilia kila siku nikikesha nikiomba labda Mungu atambadilisha lakini wapi?

Sitaki kuelezea sana niliyopitia lakini niseme tu Mume wangu hakuanza tu kunipiga baada ya ndoa, hapana alikua akinipiga hata kipindi cha uchumba. Yaani kila nilipokuwa nikimfumani alinipiga na kuniomba msamaha. Hapa pia naomba mnielewe ninaposema kupigwa simaanishi kupigwa makofi mawili matatu, namaanisha kupigwa kama mbwa.

Lakini nilikuwa nampenda na nilivumilia na kila mara aliniahidi kubadilika lakini ilimchukua muda sana kubadilika na kuacha kunipiga. Tuachane na hayo turudi katika siku ambayo sitakuja kuisahau katika maisha yangu yote na siku ambayo naijutia na iliyonilazimisha kuandika hiki ninachoandika ili kama na wewe uko kwenye hali kama yangu usisubiri ya kukute ndiyo ujutie.

******

Siku hiyo nilikuwa nimechoka sana kwani baada ya kumkaliza shughuli za pale nyumbani nilipigiwa simu kuwa Mama anaumwa, alikuwa amelazwa Muhimbili akishindwa kupumua. Alikuwa na pumu ya muda mrefu hivyo harakaharaka nilienda kumuangalia. Mchakato wa kuhangaika na madaktari, mchakato wa kuenda kutafuta dawa mji mzima ulinifanya kuchoka sana.

Nilijaribu kumpigia simu mume wangu ili kumuambia lakini hakupatikana hivyo nilimtumia meseji kuwa Mama anaumwa na kalazwa Muhimbili. Sikukumbuka tena kumtafuta kwani akili haikuwepo, mpaka usiku ule wa saa tatu natoka Muhimbili mume wangu alikuwa bado hajanipigia simu na kila nikimtafuta kwenye simu yake alikua hapatikani, sijui kwanini lakini laini zake zote mbili zilikuwa hazipatikani.

Kwa maana hiyo nilijua kua alikuwa hafahamu kuhusu Mama hivyo nikifika nilikuwa na kazi ya kujielezea na kama asingeelewa nilishajiandaa kwa kipigo. Nilifika nyumbani na kufunguliwa na mfanyakazi wa ndani, mume wangu alikuwa chumbani, tangu saa kumi na mbili aliporejea na kunikosa aliingia chumbani na hakukuwa na mtu wa kumsemesha.

Mtoto wangu wa mwisho wa miaka mitatu ambaye bado alikuwa hajaanza kumuogopa Baba yake ndiyo alikuwa anaweza kuingi chumbani lakini naye alikuwa ameshalala hivyo alikuwa apeke yake tu huko chumbani. Niliingia kwa uoga na kumsalimia lakini hakujibu. “Nilikuwa muhimbili Mama anaumwa kalazwa…” Ilibidi nijiongeleshe tu ili ajue asbabu ya mimi kuchelewa.

Lakini haikusaidia aliendelea kukaa kimya akisoma kitabu chake ambacho hata sikumbuki kilikua kitabu gani. Nilivua nguo harakaharaka ili kuingia bafuni kuoga, lakini nikiwa nimefunga khanga moja nilimuona akisimama.

“Huyo Mama yako ndiyo amekuoa, inamaana unaweza kuondoka humu ndani bila ruhusa yangu? Umefundwa wewe? Unajifanya sijui ujinga unaofanya unajifanya umetoka Hospitali! Hospitali kitu gani?” Alianza kuongea kwa hasira, nilianza kujitetea lakini ndiyo nilikua nimeuwasha moto, alianza kunipiga makofi na kunisukuma, nilidondoka chini alinifuata kulekule na kunishika nywele zangu ndefu akaanza kuzivuta kunisimamisha.

Maumivu niliyoyapata siwezi simulia, kama ni mwanamke unasuka rasta unajua ni namna gani kcihwa kinauma na kuvuta unaposuka tu sasa hembu vuta picha mtu anashika nywele zako na kukunyanyua juu juu kama karatasi. Nilishindwa kuvumilia, nilipiga kelele huku nikimsukuma, ingawa ikumsukuma kwa nguvu lakini aliteleza na kudondokea kitandani.

“Unanipigaee! Yaani unanirudishia! Umeota mapembe eeeh! Sasa ngoja nikuonyeshe!” Aliongea kwa hasira akiwa bado palepale kitandani, alianza kuvua mkanda huku akiangalia ni kitu gani kingine rahisi cha kuokota na kunipiga nacho, sijui kwanini lakini nilijikuta naanza kukimbia kuelekea sebuleni. Haikuwa kawaida yangu mara zote huwa akinipiga nakimbilia chumbani ili watoto wasione lakini siku ile nilikuwa nimechoka na nilijua kipigo chake kitakua cha mbwa.

*******

Alinifuata kule kule sebuleni na wakati nikipita nikiijaribu kufungua mlango wa nnje ilinitoke alishanifikia, alianza kunipiga makofi na kunichapa kwakutumia mkanda. Nilikua nikipiga kelele lakini hakukuwa na mtu wa kunisaidia. Nilikuwa na mfanyakazi wa ndani ambaye ni binti mdogo alikua anogopa, mwanangu wa kiume Fred ndiyo kwanza alikua na miaka kumi akifuatiwa na kabinti ka miaka sita, wote walikwa wamesimama wanaangalia tu huku wakilia.

Alinivuta na kunidondoshea kwenye kochi, kanga moja niliyokuwa nimejifunga ilivuka na kubaki kama nilivyozaliwa hakujali, aliendelea kunipiga makofi akiniinamia pale huku akipiga kelele kuwaambia watoto waingie ndani lakini Fredrick mtoto wangu hakukubali. Namaani alishachoka ile hali ya mimi kupigwa pigwa kila siku, sijui alipata wapi ujasiri lakini alienda na kuokota blenda ambayo ilikuwa juu ya meza ya chakula alikuja nayo kwa kasi na kumpiga Baba yake mgongoni.

“Muache Mama! Utamuua Muache...” Alionge akwa hasira huku akitaka tena kunyanyua kumpiga Baba yake, lakini Baba yake alishageuka aliikamata ile Blenda na kwa hasira alimrudishia kumpiga na moja kwa moja ilimdondokea kichwani. Kimya Fred alidondoka chini na damu kuanza kutiririka, mume wangu alibaki ameduwaa, nikiwa uchi vilevile nilinyanyuka na kwenda kumuangalia, alikuwa hatikisiki, macho yamemtoka, damu zinamtoka puami na mdomoni.

“Mume wangu umeua! Mume wangu umeua!” Nilianza kupiga kelele kujaribu kumuamsha mwanangu lakini hakuamka. Mume wangu nguvu zilimuishia na kukaa chini, hakusogea hata kumshika mtoto kuuangalia mapigo ya moyo, machozi yalianza kumtoka kama mtoto mdogo. Mfanyakazi alitoka nilimuamsha mume wangu ili tumpeleke mtoto hospitalini ndipo alipozinduka na kunaynyuka kwenda kuwasha gari.

Nilitaka kutoka vilevile nikiwa uchi mpaka mfanyakazi nitolea nguo nikavaa. Tulifika hospitalini na kuambikuwa ameshafariki. Hospitalini sijui nini kilifanyika kwani hakukuwa na cha PF3 wala nini, wakati huo akili yangu haikuwa sawa hivyo sikujali mambo hayo lakini nilijua wakati tunajiandaa na mazishi. Kila nilipowaambia watu kilichotokea waliniona kama kichaa kwani maelezo yaliyotolewa kua mwanangu alifariki kwa ajali ya gari.

Sio maelezo tu bali pia mfanyakazi wa ndani alisema hivyo hivyo, mashahidi wapekee niliokua nao ni mtoto wangu wa miaka sita na mwingine wa miaka mitatu. Haiishii hapo gari lililopata ajali lilikuwepo, sijui mume wangu alifanya nini lakini gari lake alilokuwa akitumia lilikuwa limeboindekabondeka kama vile limegonga mti.

Ili kuwaaminisha watu badala basi hata ya kupelekwa gereji lilivutwa mpaka nyumbani na ndani kulikuwa na damu zimegandia sijui hata zilitoka wapi kwani zilikuwa ni nyingi tena siti ya mbele wakati tulitumia gari jingine kwenda hospitali. Ilinibidi tu kunyamaza kwani nilijua hakuna namna ambavyo ningeweza kumfanya mume wangu kulipa kwa aliyoyafanya. Hakuomba msamaha zaidi yua vitisho kuwa nikisema ataniua huku akinitishia kwa kuwadhuru watoto.

Bado niko kwenye ndoa na sina pakwenda, sipo kwaajili ya pesa bali kwaajili ya wanangu. Sijui ni nini kitatokea kama nikiondoka kwani ameshakataa katakata kuniruhusu niondoke nao. Nimwaka wa pili sasa tunaishi kama kaka na dada, sina furaha na sitegemei kuipata. Nalea tu wanangu na nimeshakata tamaa ya maisha.

Nimeamua kuandika kisa changu hiki ili wanawake wengine kujua kuwa unapokubali kupigwa na mwanaume hubebi maumivu peke yako. Wanao wanaona hata kama unaficha vipi na unawaathiri, wanakupenda na wanaumeia unavyoteswa kwani wewe ni Mama yao. Hembu wewe fikiria mtu anampiga Mama yako halafu huwezi kumtetea utajisikiaje.

Simlaumu mume wangu kwa kifo cha mwanangu, halikuwa Kosa Lake. Kosa lilikuwa la kwangu kuvumilia mateso, kuona kipigo kama sehemu ya ndoa. Ningeondoka mapema, ningekataa kipigo tangu siku ya kwanza haya yote yasingetokea. Nimejaribu sana kumlaumu mume wangu lakini wapi, mkosaji ni mimi kwani mimi ndiyo nimevumilia na kumlea.

Ingawa alianza kunipiga tangu kipindi cha uchumba lakini hakuanza tu ghafla, alianza taratibu makofi ya hapa na pale na kwakua nilikuwa nikimchekea na kujaribu kumtetea huko kichwani mwangu, alizoea mpaka ikawa kitu kidogo tu haongei ni makofi. Kama ambavyo wewe kila siku unavumilia, unasema ndiyo ndoa zilivyo, unasema ipo siku atabadilika na mimi ndiyo hivyo hivyo nilikuwa navumilia kabla na baada ya ndoa.

Siku hizi hanipigi, ameshabadilika lakini haisaidii tena, haina maana tena kwangu kwani sina hisia tena za mwanaume mwili nikama umepigwa ganzi. Pumzika kwa amani Fred wangu, shujaa wangu uliyekufa ukinitetea, umekufa kifo ambacho hukustahili na yote hiyo ni kwasababu ya mimi Mama yako. Naomba unisamehe, unisamehe kwa kuvumilia ujinga, unisamehe kwa kujiangalia mimi bila kujua kuwa nilikuwa nakuumiza wewe na wadogo zako, natumaini huko uliko utanisikia na utanisamehe
Naombeni ushauri wenu nifanyeje maana kiukweli hapa najihisi kama nimekufa nipo gizani sijui nini kinaendelea sina hamu na ndoa natamani tu kuishi mpweke sitaki kabisa mwanaume yeyote moyo wangu umekufa ganzi hisia za kupenda zimetoweka moyo umejaa makovu na maumivu, majuto na majonzi yametawala akili yangu NIPENI USHAURI TAFADHALI NIFANYAJE??

Dah inauma sana karibuni kwa ushauri huo ndio mkasa uliomsibu Gloria, una lipi la kumshauri?




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz