WANAWAKE MNAKWAMA WAPI JUU YA USIMAMIZI WA NDOA ZENU? - EDUSPORTSTZ

Latest

WANAWAKE MNAKWAMA WAPI JUU YA USIMAMIZI WA NDOA ZENU?

Image may contain: one or more people, people standing, ocean, sky, beach, outdoor, nature and water

Mwanamke yadai Haya ikiwa kweli Mumeo aliapa KUKUPENDA ili kutimiza TORATI;
 MUDA.
 MAONGEZI.
Utajengaje Familia na Mtu ambaye kutwa yupo busy, Usiku anarudi saa 6 unakutwa ushalala usingizi, Mwanaume wkend zote ana udhuru, Mwanaume hana muda wa kukaaa na familia, Mwanaume hana maongezi na wewe MNAJENGAJE FAMILIA KWA PESA?
Unadhani kama familia zingejengwa kwa PESA #Billgate na akina #Alikodangote wangeheshimu wake zao?
Hujiulizi kwa #RegnardMengi kutwa akihangaika na mkewe location kupiga picha 📷 wewe hata Mumeo hana picha yako hata moja, Wewe huna picha ulipiga na Mumeo Bado unajivunia Una MUME?
Unatamba Instagram mashoga wakuone uko Kempnsik na Wanao mnaonyesha ufahari lakini MUME siraha yake WALLET💸 akiisha kupatia laki tano masikio yanakusimama ili na wewe ukawe HURU kuchat na BEN TEN ukija kushituka KUNA NYUMBA NDOGO INA KICHANGA CHA MIEZI 6 unalo hilo bibi😅😅😅
Ukimkosa Mumeo kuwahi nyumbani ULIZA tena ukiwa serious, Ukimkosa Mumeo siku za wkend HOJI tena bila kucheka, USIPOZIBA UFA SIJUI KAMA UTAWEZA KUJENGA UKUTA tena kwa kipindi hiki cha Brother John? Usije kusema sikukwambia, Janja ya WANAUME ni kujifanya wapo busy sasa zinduka tujue MBICHI na MBIVU huo ubusy gani mpaka FAMILIA INAKOSA MUDA NA MAONGEZI YA BABA? Mwanaume anayejua THAMANI YA FAMILIA YAKE ANATENGANISHA MUDA WA KAZI NA MUDA WA FAMILIA ila ukiona hayo hayaji kwa wakati ujue HAUKO PEKE YAKO.
Mungu mwenyewe katika kuitengeneza DUNIA akaweka MCHANA WA KAZI na USIKU WA MAPUMZIKO Yaani Mungu mwenyewe akajua mchana ukatafute na usiku uwe na wako MAHABUBA mkipeana ARA ZA ROHO.
Kuna familia utamjua Mama, watoto mpaka house boy na house girl ila MUME ng'oooo😂
MUME akiambata na mkewe ni kwenye gari FULL TINTED wanaweza kuwa huru ugenini, JE NI KWAMBA WEWE SIO TYPE YAKE AMA NDO WALE WALIOA KWA MIHEMKO AU SABABU baadaye wakajutia?
Wakati yeye akiona humfai ama wewe sio wa type yake kumbe amekufanya YAYA ama KUU LA WASAIDIZI😅😅😅
Mwanamke itafute AMANI yako Kwenye NDOA yako kwa sababu uliishaolewa, Kataa kuwa PAMBO LA NYUMBA YA MWANAUME.
Hii tabia yenu ya KUDAI MABADILIKO NJE YA NDOA mnajitaabisha, MABADILIKO uyadai ndani ya NDOA yako tu na ukiyakosa TAMBUA HUPASHWI KUWA KWENYE ENEO HILO maana maisha yako yatabakia kuishi kwa upweke, Unatamba UNA NDOA wakati unaishi kwa kusema AFADHALI YA JANA?
Kidonda kinatibiwa kwa dawa wala sio kwa kufunika ukiogopa NZI🐝
Usiwadanganye watu uko na NDOA YENYE AMANI KISA WANAKUONA UNAENDESHA GARI ZURI NA KUISHI GHOROFANI hayo hayawezi kukupa AMANI bali yanakupa MATUMAINI kwa sababu ya UFAHARI lakini ndani yako kunafukuta moto🔥
Siku zote NYUMBA inajengwa kwa kuanza na MSINGI je Unadhani mlivyoanza ndivyo mlivyo sasa? Chukuwa hatua KUDAI HAKI YAKO KAMA MWANAMKE achana na kudai VITU hivyo vinapita popote My Friend, Hazina kubwa ya MAISHA ni AMANI sasa ukitaka UPAUKE KOSA AMANI leo utajidanganya kwa sababu ya BEN TEN wanakutoa stress but kumbuka UKO KITANZINI.
Mapenzi nje ya ndoa ni sawa na PANADOL kwenye KANSA wala haitakupa UPONYAJI😎
Kama limebuma hilo limebuma tu, Mali sio hasara, HASARA ROHO.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria🔨
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz