GHARAMA YA UPENDO WA KWELI HUJA PINDI MTU ANAPOAMUA KUKATISHA UHUSIANO WENU😭😭 - EDUSPORTSTZ

Latest

GHARAMA YA UPENDO WA KWELI HUJA PINDI MTU ANAPOAMUA KUKATISHA UHUSIANO WENU😭😭

Image may contain: 1 person, sitting

Ni kweli MAUMIVU ya pendo💔 la kweli hayafutiki japo Kuna wakati Mtu unaweza kusahau kutokana na MAJUKUMU YA KI MAISHA ila asikwambie mtu, Kama ulimpenda kweli kweli na akaamua kukatisha PENZI hilo hayo MAUMIVU hayaishi kwa kujisahaulisha, Wala hayawezi kuisha kwa VUGUVUGU LA PEN-ZI JIPYA📛
Ujinga ni pale ambapo unamuacha Mtu aliyekupenda kwa hakika ya MATENDO eti kisa ana kauli mbaya, amekusaliti, Rafiki hapa DUNIANI hakuna mkamilifu TUNAISHI KWA KUBEBEANA MADHAIFU YETU unapoamua kumuacha Mpenzi wako kwa mambo ambayo HATA UENDE WAPI UNAWEZA KUKUMBANA NA KADHIA HIYO HIYO huo ndo ujinga rasmi, Mimi nadhani Bora uniambie kwamba HAKUPENDI ndo umeamua kukatisha uhusiano ninaweza kukuelewa, Ila kama unamuacha kwa USALITI kumbe MALAIKA UNAMPATA WAPI? Ikiwa Mungu mwenyewe alisema kwamba HAKUNA MWANA WA ADAM ALIYE MKAMILIFU sasa huyo wako mkamilifu amezaliwa DUNIA ipi?
Kosa kama USALITI you need to fight 👊 ili kama amesaliti kwa kutaka uondoke okay just leave💃
Kosa la UROPOKAJI nalo likuondoshe kwa mwenye TRUUUE L0VE? Pengine kuropoka kwake ndo UPENDO wake kumbe unashindwa nini kumzoea mkaendelea ikiwa ANAKUPENDA?
Rafiki utatanga kiguu na njia kumtafuta MALAIKA wala usimuone, Wakati huo utakuwa unaongeza namba tu ya mahusiano, Na usiponzwe na MANENO MATAMU awali Siku zote ina radha zake ila ukiingia ndo utajua MBIVU NA MBICHI😅😅
Watu wengi wanajilisha upepo eti akiumizwa kidogo tu Huyoooooo💃 anakwenda kusaka UHUSIANO mpya kwa kutaka kubembelezwa, Wakati mkiisha peana MDINYO tayari MNAKUWA ZILIPENDWA😅😅
Hakuna THAMANI kama kuboresha UHUSIANO wako ulioujenga kwa muda mrefu na UNAUPENDA hata kama kuna mapungufu STAY STRONG💪
Bora MWENYE UPENDO WA DHATI ila Mjinga, Kuliko MWENYE AKILI lakini hana UPENDO WA KWELI.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria🔩
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz