1. Daima kuwa muwazi na mkweli kwa mwenzako.
2. mtegee sikio mwenzako. Huwezi kujua anachokitaka bila kumsikiliza au kumtegea sikio.
3. Ndoa yako inapaswa kuwa kipaumbele chako. Inapaswa kuwa nafasi ya kwanza kabla ya chochote.
4. Daima muulize mwenzako maswali kwa NAMNA bora iwapo unahisi kuwa kuna jambo haliko sawa. Usijifanye kuwa mambo yako shwari wakati sio kweli. Kufunika hisia zako sio jambo zuri, muhimu ni kujua namna bora ya kujieleza.
5. Zawadi ni kitu kinachoulainisha moyo wa mtu na kumjaza hisia za upendo. Hivyo, usipuuze suala la kumnunulia zawadi mwenzako hata kama ni kidogo. Fanya hivyo mara kwa mara.
6. Usichoke kusema “NAKUPENDA”. Mwambie “NAKUPENDA” mara nyingi kila siku kadiri iwezekanavyo.
7. Jifunze namna bora ya kuongea na mwenzako kwa faida ya ndoa yenu bila kumuumiza.
8. Fanyeni tendo bora la ndoa. Msiliache. Lifanyeni mara kwa mara. Huwezi kuwa na ndoa imara bila tendo la ndoa.
9. Tengenezeni utaratibu wa kula pamoja kadiri iwezekanavyo.
10. Usitengeneze visingizio vya kuacha kuwa pamoja na mwenzako. Tenga muda wa kutosha kusuhubiana na mwenza wako.
11. Tengenezeni utaratibu wa kukoga pamoja.
12. Mheshimu mwenza wako.
13. Fanya juhudi za kujali muonekano wako. Mwenzako anapenda uwe na muonekano maridhawa muda wote.
14. Kubali makosa yako unapokosea. Acha kuishi katika mfumo wa kujifanya kuwa huwezi kukosea na kujivika joho la utakatifu.
15. Msamehe mwenzako anapokosea na epuka kuibua makosa yake yaliyopita. Wanandoa mahiri hawachoki kuwasamehe wenzao mpaka wanaingia kaburini.
16. Ongea zaidi na mwenzako. Weka simu chini, zima televisheni na uwe na maongezi maridhawa na mwenzako.
17. Ushike mkono wa mwenzako mnapokuwa mnatembea au mnapokuwa mumeketi.
18. Tengeneza utaratibu wa kumbusu mwenzako mara kwa mara, hasa mnapoagana na mnapokutana. Busu huongea maneno elfu.
19. Muandikie ujumbe wa mahabba mara kwa mara.
20. Daima sema “AHSANTE” na “SAMAHANI”.
21. Yakubali mazuri na mapungufu ya mwenzako.
22. Mstahmilie na umvumilie mwenzako.
23. Epuka jazba unaposhughulikia changamoto yoyote katika ndoa. Mihemko hukufanya husahau kuwa mwenzako ndio kila kitu kwako.
24. Epuka kugombana kwa kila jambo. Wakati fulani ni bora kuacha baadhi ya mambo yapite.
25. Ufanye ulimi wako kuwa kitovu cha faraja kwa mwenza wako. Lugha inayopenya moyoni huonesha kuwa wewe ni mtu wa kipekee. Uzuri wako uko chini ya ulimi wako.
26. Cheza na mwenzako, furahi pamoja naye, mtanie kwa matani na mzaha usiomuumiza.
27. Usimpuuze na kumdharau mwenzako.
28. Usifanye vitu ambavyo unajua vitamuumiza mwenzako.
29. Tumia neno “SISI” badala ya “MIMI”, kwa maana huonesha mshikamano na umoja wenu.
30. Msifu mwenzako kila siku.
No comments:
Post a Comment