USIRUHUSU MANENO YAKAUHARIBU MOYO WAKO - EDUSPORTSTZ

Latest

USIRUHUSU MANENO YAKAUHARIBU MOYO WAKO


Maneno n mengi na Huwaga Yanatokana na wanadamu ambao wengi hawapendi maendeleo yako na ambao hukesha kupanga mipango ya uharibifu Kwaajil ya maisha yako
Maneno Huwezi kumzuia MTU kuongea Ila unaweza kuyazuia kuingia kwenye Moyo wàko hayo maneno
Mwanadamu kwakuwa Halipii Kodi mdomo wake bas kuongea anaweza kuongea Tu hivyo huwezi kumzuia kuongea .....
Maneno n mfano wa maji Baharini Acha nikuambie Jambo moja zuri Sana
Ukiwa na chombo Baharini na ukawa unasafiri pale utaruhusu Maji kuingia kwenye chombo bas ndivyo ambavyo utazama na Utashindwa kufika kwenye Safar yako
Lakini pia Kumbuka maji hayo hayo yanatumika kukusafirisha wewe na kubeba chombo chako
Maneno yanaweza kukuzamisha kama ukiyaruhusu kuingia kwenye Moyo wàko
Lakini pia maneno hayo hayo ndio yanaweza kukubeba kukamilisha safari yko
Maneno yapo ili wewe uwe mshindi
Kama wasingekusema kwenye nyumba za kupanga usingewaza kujenga Nyumba yako Hapo yametumika kama Njia ya wewe kufanikiwa kwenye maisha
Usiyaogope maneno
Usiogope wanaoongea Kwaajil yako
Usiogope wanaokusema wanakaa mpaka vikao Kwaajil yako
Debe tupu ndilo lenye makelele
Debe lenye kitu Huwaga halipigi kelele
Bwana atakupigania nawewe utanyamaza kimya !!!!!!....
Waache wapige kelele wao n Debe tupu pambana Kwaajil ya hatma yako
Maana Mungu anatazama jitihada zako apate kukubariki
....... USIKATE TAMAA KWAAJIL YA MANENO YAO ....MUNGU ANAKUWAZIA YALIO MEMA
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz