Usimlaumu mtu kabla ya kuchunguza, fikiri kwanza halafu utoe lawama, sikiliza kabla ya kujibu. - EDUSPORTSTZ

Latest

Usimlaumu mtu kabla ya kuchunguza, fikiri kwanza halafu utoe lawama, sikiliza kabla ya kujibu.


Mwanamke au mwanaume anapochoka mapenzi ya kitoto na kupewa ahadi hewa mwisho wa siku hutafuta pumziko lenye tija katika mustakabali wa maisha yake na future yake.
Ubunifu wa mapenzi daima hutokea sehemu yenye mapenzi ya dhati na sehemu ya kuaminiana.
Baadhi ya vijana linapokuja swala la mapenzi, utoto umechukua sehemu kubwa sana. Ndio maana mabinti wengi wameingia kwenye mauhusiano na wanaume wenye kujitambua na nidhamu ya kila kitu na sio kutizama umri wala kazi.
Mke mwaminifu ni furaha ya mumewe; mumewe ataishi kwa amani miaka yote, na ndoa zote tamu zina misingi mizuri ya uchumba.
Chunga moyo wako na ubongo wako katika swala zima la mahusiano/huwezi tenegeneza future nzuri au kuwajibika ukiwa heartBroken.
Baadhi ya wanawake pesa ndio imekuwa kigezo kikubwa sana katika kutengeneza mahusiano,tumia akili kutafakari kuhusu ndoa na usitumie moyo kifikilia ndoa, pesa haiwezi kukupa furaha ya ndoa.
Angelina Jolie na utajiri wa $200 Million ndoa imemshinda. Jenifer Lopez anabadili wanaume kila uchwao pesa anazo ila mapenzi ya dhati hapati.
Chagua mwanaume kwa upendo wake wa dhati ili aku treat kama princess na usichague mwanaume mwenye pesa akutreat kama Housegirl.
Dear brothers mwanamke bora na mjenzi wa familia hatizamwi shape, sura wala rangi. Uzuri wa mwanamke upo kwenye ubongo, moyo wake tabia yake na ushauri na maono yake yenye tija anayokueleza kipindi cha uchumba wenu.
Kuna mambo ya msingi ambayo mwanamke ambaye ana ndoto za kuwa mlezi wa familia hatayafanya kipindi mpo katika uchumba.
Mwanamke asie na ushauri wala mawazo mtambuka ni mzigo ambao wewe kama mwanaume unaweza kukuelemea huko mbeleni.
Wanawake bora hutengeneza wanaume bora ila usiwekeze kwenye figure namba 8 ukataraji utapata ndoa bora. Muombe Mungu akupe mke bora.
"Money does not buy happiness but, it sure pays off stress. Don't marry the person you think you can live with; marry only the individual you think you can't live without."
Think Big, Go Big.
Share
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz