Usilazimishe kila mtu uliyekutana naye katika maisha yako ya MAPENZI awe wako milele. - EDUSPORTSTZ

Latest

Usilazimishe kila mtu uliyekutana naye katika maisha yako ya MAPENZI awe wako milele.


Wapo watu watakuja maishani mwako kukujenga kiakili na kifikra
Wapo wengine watakuja ili kukufundisha namna ya kuishi na mwenza wako
Wapo wengine watakuja ili kukupa mbinu za kumdhibiti mwenza wako kimahaba
Kuna wengine watakuja kukuimairisha kinafsi ili moyo wako usiishi kwa mateso baadae..
Lakini pia wapo ambao watakuja ili kukufanya uijue thamani yako ingawa wanaweza kuwa wa kupita tu...
KWA HIVYO, Unalo jukumu la kukubaliana na majira ili kuweza kumpata yeye huyo atakaye kukuta umekomaa kiakili na mwenye ufahamu.
Unaponyanyasika sana kwenye mapenzi jua uko shuleni, kubali kufundishwa ili baadae uweze kuwa mhitimu.
Inaumiza sana kuona uliyempenda yeye alikuwa na sababu zake kwako LAKINI haina maana kuwa huwezi kumpata mwingine
Ziko nyakati ngumu zimeandikiwa kwako lakini kwa imani yako kuna nyakati nzuri zitakuja na utasahau yaliyokuumiza.
Kubali
kudharaulika ili uheshimiwe,
Kubali
Kutupwa ili uokotwe,
Kubali
Kutemewa mate ili aje wa kukuosha,
Kubali
Kushushwa thamani yako ili ushikwe na kupandishwa juu na wajuao thamani yako.
Si kila aliyesema NAKUPENDA alimaanisha, wengine walisema ili KUKUPUMBAZA.
LAKINI nikutie moyo haijalishi umeumizwa mara ngapi, umelia mara ngapi MTUMAINIE MUNGU, HAKUNA LA KUMSHINDA.#MkakaFulani 🇹🇿
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz