THAMANI YA MWANAMKE NI NINI:? - EDUSPORTSTZ

Latest

THAMANI YA MWANAMKE NI NINI:?


Image may contain: 1 person
MWANAMKE, akilala na hali mumewe amemkasirikia, basi hulaaniwa na Malaika usikukucha.
🌼Lakini sikujuwa kua kuna na kinyume chake.
Ilitokea katika khutba ya Ijumaa, lilitokea jambo ambalo si lakawaida, jamaa mmoja alimshitaki mkewe kwa Shekhe wa msikiti mbele ya watu..

SHEKHE akamjibu kua mwanamke hubeba jukumu kubwa la nyumbani kwake... na kuyavumilia mambo mengi kumshinda mwanamume, kwa mara zaidi ya mia na mia, na hata lau angekua huyo mwanamume ana misiba au matatizo mengi na akasubiri, lakini subira za mwanamke ni kubwa zaidi..

HAPO hata sauti ya huyo Shekhe ilianza kubadilika alipokuwa anamsemesha huyo mwanamume alomshitaki mkewe na kumwambia:
Mkeo amebeba mambo yako na ya watoto wako, na anasimama kwa miguu yake kuwatengezea chakula chenu. Na Mtume (s.a.w.) ameshausia hivo.. Jee kwani hana haki yeye ya kuheshimiwa? Na ya kuthaminiwa? Bila ya kumpunguzia chakula au kitu chochote anacho kihitaji?

BASI naapa Wallahi lau mwanamume anamkasirisha mkewe, akamgeukia na kumpa kichogo akatoka nyumba kumwacha mkewe na huzuni, basi Mwenyezi-Mungu anamlaani kwa kila khatwa anapokwenda, na kumyimia rizki yake, na kumpunguzia afiya yake, na kumuandikia kwa kila chozi moja linalotoka machoni mwa mkewake huyo..
makaa ya moto elfu moja kila siku, nusu yake duniyani, na nusu kesho akheera..

NATAMANI maneno haya yawafikie wanaume wengi walokwisha owa...
Machozi mangapi mengi yashamtoka mke wako na wewe hata hujali kabisa, wala huna hamu ya kitu chochote, wala hutaki kujua habari yake..
Musiyawache maneno haya kubakia moyoni mwenu tu, bali kila mtu awatumie walokwisha owa. Na ambao hawaja owa wahifadhi maneno haya msitari msitari kama akiba ya kesho yake watakapo owa..

AMESEMA Amiir Talaal Ar-Rashiid, Mungu amrehemu,:
(( Kama aliumbwa mwanamke kuwa ndege angekuwa ni "Tausi", na kama aliumbwa kuwa mnyama angekuwa ni "Paa" (Ghazala),
na kama aliumbwa kuwa mdudu angekuwa ni "Kipepeo" (Butterfly), lakini ameumbwa kuwa mtu, kwa hivo yeye ndiye Mpenzi, na ndiye Mke, na ndiye Mama bora, na ndiye Neema nzuri kabisa ya mwanamume katika duniya hii..

Na kama hangelikuwa mwanamke ni kiumbe bora na kikubwa sana, Mungu hangemfanya kuwa Huril-ayn na kutuzwa watu Waloamini kesho Peponi.
Hakika nimependezewa na Mwanamke kwa kuwa: "Ni kiumbe ambaye unaweza kuishi naye kwa urahisi na vilevile kwa vigumu kabisa, unaweza kumridhisha kwa ua moja la waridi, na unaweza kumuuwa kwa neno moja..

JITAHADHARI ewe mwanamme ujue kuwa mwanamke ameumbwa kwa mfupa wa ubavu wako si kwa mguu wako hata umkanyage...wala si kwa kichwa chako hata umpandie juu ya kichwa chake, lakini ameumbwa kwa mfupa wa mbavu zako ili umueke ubavuni mwako, na ni kwa mfupa ulioko karibu na moyo wako ili upate kumpenda..
Mwanamke ni kiumbe bora kabisa...
Katika utoto wake humfungulia babake mlango Peponi...

NA katika ujanajali wake humtimizia mumewe dini yake...
Na anapokuwa mama, Pepo huwa chini ya miguu yake...
Maneno mazuri kabisa.....
Nampa salamu na pongezi kila ambaye ni Mwanamke mwenye sifa njema...
Shukran kwa kila atakaye yasoma maneno haya, na kila atakaye yatuma kwao wanawake na akaingiza furaha katika moyo wa kila msichana, na kila ndugu wa kike, na kila mke, na kila mama...

MOLA WETU tupe kutoka kwa wake zetu watoto wenye kukuabudu na kutenda mema pia kufurahisha macho na nyoyo zetu...Amin.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz