SOMA KWA UMAKINI SANA HII ITAKUSAIDIA. - EDUSPORTSTZ

Latest

SOMA KWA UMAKINI SANA HII ITAKUSAIDIA.


Fikra zangu zinaniambia kuwa ilikuwa ni jumatatu mwanzo kabisa wa 'week' hii, jioni nikitoka katika mihangaiko yangu huku nikisikiliza redio fulani juunya janga la colona, ndipo nilipo-sikia mlio wa 'Message' katika simu yangu, kwa vile nilikuwa naendesha gari ikabidi niliweke kando kisha nifungue simu niangalie ujumbe huo.
Ile kufungua simu tu, nikakutana na ujumbe ambao mpaka dakika huu wajirudia kichwani mwangu kila ninapo-fumba macho yangu. Ilikuwa ni namba ngeni, sikushtuka sana maana namba zangu wengi wanazo na ni kawaida kupokea namba ngeni kila siku.
Kwa maelezo yake ni dhahiri kuwa alikuwa mwanamke, alianza kwa kujitambulisha na kunisalimu kama kawaida, kisha akaanza kuniambia yaliyo-msibu mpaka kufikia hatua ya kunitafuta.
Aliniambia, "Kaka, kibonde samahani sana! Mimi ni binti wa miaka 25, sijaolewa japo naishi na mwanaume kama mke na mume kwa muda wa miaka 3 na mpaka dakika hii naandika ujumbe huu nipo kwake na nina mimba yake."
Akaendelea kwa kuniambia, "Mimba yangu ina miezi 7 mpaka sasa, ajabu ni kwamba nimekuja kugundua juzi kuwa huyu mwanaume ninaye ishi naye aliwahi kuoa na kuzaa na mwanamke mwingine, lakini mpaka leo hii hakuwahi kunifahamisha."
Nimefumania 'Texts' akiongea na mama wa mtoto wake huyo, na nikamwambia, ajabu alikuwa mkali na kuniambia sawa kazaa lakini hayupo pamoja tena na mwanamke huyo, lakini ukweli ni kwamba inaonekana bado wana mahusiano.
Baada ya ugomvi mkubwa baina yetu, akafikia hatua ya kuniambia nirudi kwetu nikazae na mtoto akikua nimpelekee, Kaka yangu mimi sina wazazi nirudi kwetu na mimba hii, nitafikia kwa nani? Mwanaume naona kanitafutia sababu na hanitaki tena! Nahitaji ushauri wako Tafadhali." Alimaliza.
Na mwishoni alimaliza kwa kusema naomba unipostie kwenye kurasa zako ....ili nipate ushauri wa wadau..... 🙏
Nami nawakilisha kama.alivyoomba
Counsellor
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz