PETE sio NDOA - EDUSPORTSTZ

Latest

PETE sio NDOA


Wadada walio.wengi hufurahia kuvishwa PETE za uchumba na mda wote kutembea wakiwa wametanua vidole ili ionekane.wengine hupiga picha kidole chenye pete na kusambaza ktk mitandao ili tu apate comments na likes nyingi..lakin mwisho huishi kulia hata kabla ya Ndoa
Soma hiki kisa kifupi
Naitwa Gwantwa ( sio jina rasmi) awali nilikuwa na kijana ambae alionesha kunipenda sana na mda mwing alikuwa ana nikumbuka iwe kunipigia simu au kutuma sms za kawaida.
Alikuwa ni mtu ambae nimefahamiana nae tu mtandaoni na sikuwah onana nae. Lakin namna mawasiliano yetu yalivyo kuwa mazur niliridhika.
Yule kijana mara zote alinipa mikakati yake kuwa lengo kunioa nami nilifurahi. Wakat huo mimi nilikuwa MWANZA yeye KIGOMA na tulipanga kuonana ili tufahamiane.
Wakat nasubir kijana ajipange ili tuonane ,nakumbuka kuna siku nilimpa taarifa ambazo hakushituka ila alishangaa pale nilipo muambia kuwa naomba tuachane kwa sababu nshampata mwanaume ambae yupp tayar kuja kujitambulisha kwetu.
" una maanisha kuwa kipind una wasiliana na mimi na unasubir kuonana na mimi kuna mwanaume ulikuwa nae??
Ina maana nilipo kuambia tutaonana kufahamiana na baadae kuishi wote hukuniamiFunzo
Kwa nn hukusema mapema kuwa una tuchanganya,,?*"
Abraham alilamika ktk sms aliyo nitumia niliisoma huku nikitokwa na machozi ..nilijihisi mkosaji ila nilipuuza na kumjibu
" kiukwel naomba tu unisamehe Abuu sikuwa na jinsi,huyu ni mtu ambae namfaham tuna kaa wilaya moja tofaut na ww upo huko mbaaalii na sijawah kuona. Mara nyingi mapenz ya mtandaon huisha bila hata kuonana.. ...nisamehe bure kukupotezea mda wako."
Zilipita dakika tano bila Abuu kujibu kisha akinipigia na kusema maneno machache kwa njia ya maswali
"Huyo mtu una muamin kweli ni Muoaji? Au kwa kuwa amekutamkia ndoa bas umepagawa?"
" sio hivyo abuu,ameshanivisha pete na wiki ijayo anakuja kujitambulisha kwetu"
"GWANTWA??"
"Nakusikia Abuu"
" kwan wangap huvishwa pete za uchumba ila huvuliwa nguo za ndan kisha kuachwa na mimba au magonjwa bila ndoa?. Sawa sitak nikupinge na siwez kukulazimisha unipende ila kuwa makin na maamuz yako ..Kuanzia leo sitakusimbua tena kila la heri ukifanikiwa"
Abuu alikata simu na toka pale sikuongea nae tena.
Baada ya mwaka kupita ktk kipindi fulani cha TV kinacho rusha mambo ya harusi niliweza mshuhudia Abuu mwanaume ambae alinipenda pasipo kuniona zaid ya picha akihojiwa juu ya bibi harusi wake.
Mtangazaji: Bwana Abuu wambie watazamaji mwanamke wako ulimpata vipi?
ABUU: kiukweli nilikutana nae facebook ktk group moja la mambo ya mahusiano .tuliwasiliana messenger kwa miez 3 tukapeana namba za simu kisha mapenz yakazaliwa mimi nikiwa Dar yeye akiwa Mwanza.
Baada ya miez 7 kupita tangu tuonane fb tuliamua kuonana uso kwa uso.nakumbuka alikuja kwangu na kukaa wiki kisha tulienda kwake kukaa wiki pia.. Miez 2 iliyo fuata tulifanya taratibu za posa na mahari. Na hivi ndo harusi yetu siku 3 zijazo.
MTANGAZAJI: una nn kuwambia wale ambao bado wanasubir upepo wa kisuli suli uvume kwao
ABUU: mapenz ya dhat yapo popote na huzaliwa popote kikubwa uvumilivu na uaminifu.. Usiogope kumpenda mtu kisa yupo mbali ukiamin huwez onana nae.
Zaman watu walipenda kwad salama za radio au magazet ambako huoni picha ya mtu na walikutana. Leo hii utandawaz picha unaona usipo ridhika nae unakaa kando "
Niliamua kuzima TV pale nilipo jiangalia ktk kidole changu nikiwa bado nina pete lakin mwanaume ambae alinivisha kumbe alikuwa amesha toa mahar sehem nyingine hivyo aliniacha miez 4 tangu anivishe pete....niliwaza meng sana na kujikuta nikisema kwa sauti
_" nilipaswa nikuamin Abuu niskkurupuke kukuacha kisa nimeahidiwa kuvishwa pete.siku 3 zijazo nilipaswa mi ndo nifunge ndoa nawe, Mungu akusaidie nimejifunza kupitia ww.. Ukawe mume bora kwa mkeo"

Jifunze kumvumilia mtu huenda ni kweli ana nia na wewe ila mambo yake kiuchumi ndo tatizo. Muheshimu sana mtu ambae ameamua kukupenda bila kufikiria ngono maana yupo mbali kuliko yule wa jiran ambae kila atapo kuhitaj kingono anataka uende.
Mapenz ni fumbo
Hivyo kuwa makin ktk kufanya maamuzi na kujua nan wa kumpa mda na hisia zako.
Kuna wakat usiye mfaham wala kumuona huweza kukuvutia na kuwa mtu muhim kwako wa kukufanya utaman kupenda tena kuliko mtu wa jiran unae muona kila siku ila kila mara maudhi.
Heshimu mahusiano yenu
Muheshimu anae kuthamin
Usiyachezee kamali mapenz
Eti kuwa nao 2atakae anza ndo huyo
Ongea na moyo wako sio tamaa ya macho na mwili kupendeza.
Kuvishwa pete au kumvisha pete kusikupe kiburi ukajiona umeshinda, wapo walio achwa siku ya harusi wengine fungate.
Wangap wamevishana pete na hawakufanikiwa kuoana?
Punguza nyodo kaka na dada
Furahia ndoa sio pete
Kuna walio vaa hizo pete mpaka basi ila hakuna ndoa iliyo tokea
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz