*💐💐PAPASO LA LEO*💐💐 - EDUSPORTSTZ

Latest

*💐💐PAPASO LA LEO*💐💐

Image result for mapenzi wakubwa
1🌻. Pandikiza katika moyo wa mwenzako uwezo wa kujiamini na kukuamini. Nawe pia muamini na umfanye ajikubali.
💖💖💖💖💖💖💖
2.🌻 Furaha yako katika ndoa haitegemei tu kuoana na mtu sahihi, bali wewe pia unatakiwa kuwa mtu sahihi.
💖💖💖💖💖💖
3🌻. Usafi ni alama ya umaridadi na mahabba.
💝💝💝💝💝💝💝
4🌻. Wakati fulani unatakiwa kuachana na baadhi ya mambo unayoyachukulia kuwa ni sehemu ya shakhsia yako, ili uweze kufurahia mambo unayoyapenda kutoka kwa mwenza wa maisha yako.
💝💝💝💝💝💝
5.🌻 Mjali mwenza wa maisha yako kama unavyojijali. Mpendelee yale unayojipendelea.
💖💖💖💖💖💖
6🌻. Ndoa inahitaji kupokea na kutoa... Tengenezeni mazoea ya kuelewana... Usiwe mbinafsi ukataka upewe zaidi ya unachotoa au kuchukua kila kitu bila kutoa chochote.
💝💝💝💝💝💝💝
🌻7. Mwanaume anataka mwanamke wa mfano anayeshughulikia mambo yote kwa umahiri, anayempa heshima, upendo na kumjali. Na mwanamke anataka mwanaume awe imara ambaye anaweza kumtegemea, kukidhi mahitahi yake na amhakikishie kwamba yeye ndiye mwanamke wa pekee na wa mwisho katika maisha yake yote.
💖💖💖💖💖💖💖
8🌻. Usifanye haraka kumtuhumu mwenza wako kila linapotokea jambo, litazame jambo hilo kwa jicho la uadilifu bila papara.
💖💖💖💖💖
9🌻. Ishi leo, usiwaze mambo ya kesho ambayo haijakufikia... Ishi ndani ya mipaka ya uwezo wako.
💖💖💖💖💖
🌻11. Utambue utukufu wa ndoa na kwamba ndoa ni mafungamano mazito. Fikiria mara elfu kabla hujachukua hatua ambayo utaijutua. Siku zote majuto ni mjukuu.
🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻 ðŸŒ»ðŸŒ»ðŸŒ»ðŸŒ»ðŸŒ»ðŸŒ»ðŸŒ»ðŸŒ»
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz