Muda mwingine unatakiwa kufunga ukurasa na kukubali kwamba KITABU CHA MAISHA YAKO KINAENDELEA pamoja na hayo unayopitia - EDUSPORTSTZ

Latest

Muda mwingine unatakiwa kufunga ukurasa na kukubali kwamba KITABU CHA MAISHA YAKO KINAENDELEA pamoja na hayo unayopitia

.Image may contain: one or more people and outdoor
Kwa sababu ukisimama kwenye ukurasa mmoja utashindwa kujua ukurasa unaofuata una maana gani katika kitabu cha maisha yako, Pengine ulipo unapitia magumu kiasi unakata tamaa na kujihisi huna THAMANI TENA hata ukajikuta unaumia sana FUNGA UKURASA HUO.
Usiusome tena, ni ngumu kuelewa lakini kubali kuufunga na ufungue ukurasa mwingine, Usitumie Muda na siku zako kujaribu kujisahihisha kwa yaliyopita, Bali unaweza kujivika ujasili kwa hayo, Yaache yapite yaliyokuumiza ili uruhusu MUNGU kukutengenezea kitu kizuri kwa mafanikio yako.
Ni kweli KILICHO ZOELEKA MOYONI KUKIONDOA NI GHARAMA na mtu usipokuwa makini hapo ndipo kale ka wimbo ka SAIDA KALOLI;
"Mapenzi kizunguzungu" katasikika masikioni, akilini mwako.
Lakini kinachoweza kukuponya na kukupa KUSONGA mbele ni baada ya wewe kukubali kwamba ulikuwa na Mtu ambaye hakuwa SAHIHI KWAKO.
Kwa sababu Mtu sahihi anajua nini maana ya yeye kuwa na wewe hivyo hawezi kujaribu ukose AMANI.
Kwa sababu Mapenzi yanamtaka mtu kuwa IMARA kulitetea penzi lake kuliko kufurahia penzi husika, Kulia hakukupi KUPONYA JERAHA ZAKO bali unamaliza uchungu moyoni na tatizo kubaki palepale.
Vaa ujasili, Vaa ugumu, Vaa uthubutu pamoja na KUJIVIKA NGUVU YA KUKATAA KUWA MNYONGE Kwani wewe ni wa THAMANI💪
Ulimpenda, Ulimthamini, Ulimpa kila kitu lakini hayo hayana THAMANI KWAKE ndo maana haogopi kukupoteza😭😭😭
Kubali sasa kwamba huyo sio wa kwako NIAMINI HUO NDO UKOMBOZI WAKO💪 na kwa hakika WEWE NI MSHINDI ikiwa utajua kukabiliana na YALIYOKUUMIZA.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria🔨
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz