MKATAE MTU ANAE KUFANYA KITAFUNIO🥐 KWANI ANAKUPOTEZEA MUDA WAKO! - EDUSPORTSTZ

Latest

MKATAE MTU ANAE KUFANYA KITAFUNIO🥐 KWANI ANAKUPOTEZEA MUDA WAKO!

Happy young interracial loving couple hugging and smiling at home, looking at camera. Stock Photo - 37393849

Ni rahisi kuinywa chai kavu kuliko kula kitafunwa🥖 bila chai🍵 au maji🥛 Kwanini nasema hivyo🤷🏽‍♂ Mtu anapokufanya wewe wa mpito maana yake wewe sio lazima utembee nae kwenye maisha yake, Yaani hata usipokuwepo yeye maisha yake yanasonga, Ni hatari kukutana na mtu ambaye kwa akili yake ameji-tune kuwa nawe kwa sababu zake tu wala sababu hizo hazimfanyi asiendelee bila wewe, Unajua siri iliyoko ndani ya MOYO wa mwenzio ni ngumu sana kuijua, Maneno matupu hayaleti uhalisia wa yaliyojificha ndani yake, Leo nataka nikutofautishie Kati ya mambo matatu muhimu kwenye MAHUSIANO;
■ KUJITOA
■ KUSHIRIKI
■ MUDA
Nitachambua kwa ufupi sana ila naomba unielewe, KUJITOA ni kumtekelezea MwenZio kile anahitaji, Mtu akijitoa anaweza kutajwa ni MOYO kwa kufanya hivyo, KUSHIRIKI ni kuwa upande wa kile ambacho kiko mbele ya mwenzio, Mtu anaposhiriki jambo la mwenzie maana yake anatajwa kuwa na MOYO kwa kutenda hilo, MUDA ni kusimamisha ya kwako ili uwe na mwenzio na kwa tendo hilo ni MOYO umemtuma kutenda hilo... Yote ni Mazuri kati ya hayo lakini lililo na nguvu kuliko yote ni moja tu KUSHIRIKI! Mtu anaposhiriki ujue KAJITOA Kwani huwezi kushiriki bila kujitoa ushiriki, wala huwezi KUSHIRIKI bila MUDA kwa maana hiyo huwezi kushiriki bila kuwa na Muda, Ni nani AMESHIRIKI NAWE?
Kumpata ambaye atashiriki nawe maana yake atakupa MUDA WAKE Lakini pia ATAJITOA KWAKO... Pendelea zaidi mtu wa KUSHIRIKI kuliko anaejitoa bila kushiriki maana wengi hujitoa wala wasishiriki, Ni bora ashiriki ndani utaona kujitoa na atakupa Muda wake, Kataa kuwa kitafunwa Kwani HUWEZI KUONA AKISHIRIKI ila kwa sababu zake anaweza KUJITOA kwa sababu anazo sababu zake.
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria 🙋🏻‍♂




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz