MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU "MWANAMKE" - EDUSPORTSTZ

Latest

MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU "MWANAMKE"

Image may contain: 1 person

Baada ya Mungu kumuumba Adam akamuona amekua mpweke sana ndipo akaamua kutumia sehemu ya ubavu wa Adam kumuumba mwanamke wa kuwa nae yani Eva. Hii ina maana kuwa maisha ya mwanaume hayawezi kukamilika pasipo mwanamke pembeni, maana mwanamke ni mfariji, mliwazaji, mshauri, mlezi na msaidizi mkuu wa maisha na familia kwa mmewe. Hii ndio maana ya awali ya mwanamke na sio CHOMBO CHA STAREHE kama anavyoonekana miaka hii.

MJUE MWANAMKE

Mwanamke akitabasamu muda mwingi paji lake la uso huionyesha AMANI aliyonayo moyoni, Mwanamke aweza kuwa na furaha juu ya maisha yake Binafsi lakini ikiwa atakosa Mtu sahihi wa kumfanya awe Mwanamke ni nadra sana kumkuta Mwanamke akiwa na uso wenye NURU... Alivyoumbwa Mwanamke ni tegemezi wa furaha kutoka kwa mwanaume, Kosa kubwa lililopo kwa Mwanaume ni kumuona mwanamke kama chombo fulani, Mwanamke napenda kumuita ni MHANGA WA MAPENZI maana mwanamke mara nyingi huwa hapendi kwa mpito bali akiamua KUPENDA anapenda kwa muendelezo, Mwanamke ni mwepesi kudanganywa lakini pia Mwanamke ni mwepesi kujuwa kama amedanganywa na kwakuwa analo PENDO la kweli Mwanamke ni mwepesi kuibeba DHAMANA ya kulitetea penzi lake japo amebaini amedanganywa... Mwanamke aweza kuishi kwa upendo na Mwanaume muongo na wala Mwanaume asijue, Mkosi alio nao mwanamke NI KUUMBIWA MWILI WENYE MATAMANIO KIASI WANAUME WANAZINI NAE HATA HAJAVUA NGUO lakini hapohapo namsema mwanamke anayo BARAKA kwakuwa ameumbiwa kitu ambacho bila hicho wanaume wangekuwa si waongo maana uongo wa mwanaume ni pale anapohitaji TUNDA LA MWANAMKE! Mungu alipomuumba ADAM alimuweka duniani kutokana na kumuona mwenye mno ndipo alipomuumba EVA kuja kuwa mfariji mkuu , Kwa maana fupi MWANAMKE NA MWANAUME tunategemeana sana japo utegemezi wa Mwanamke kwa mwanaume Una VIWANGO ila utegemezi wa mwanaume kwa mwanamke umetawaliwa na tamaa, Ni wajibu wetu sote wanaume KUMTAZAMA UPYA MWANAMKE ILI KUMPA MAANA YA YEYE KUUMBWA KUPITIA MBAVU ZETU.

mwanamke ni mwepesi kuzoea, Akipenda hujivunia kuwa nawewe! Haoni aibu kusema ANAKUPENDA japo ni mwoga kujiachia kwako, Wewe ni sababu ya udhaifu alioumbiwa hivyo uwe mwepesi kukabiliana na udhaifu huo... mwanamke akijuwa UNAMPENDA yupo tayari kuhama kwao, Akikupenda huyadhibiti macho yake yasimtazame mwingine, Lakini pia hasikilizagi la mtu ikiwa ameridhia kuwa nawe, Tumia akili zako KUMTULIZA! Mikono yako ndiyo yenye uwezo wa kumpa usingizi

Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz