HESHIMA YA MWANAUME NI...! - EDUSPORTSTZ

Latest

HESHIMA YA MWANAUME NI...!

Image may contain: 2 people

Heshima ya mwanaume ni kuyasimamia majukumu yahusuyo mwanaume ili kuileta maana ya mwanaume... Mwanaume akiwa MUME anazo jitihada za kuilinda na kuipa mahitaji ndoa yake, Maisha ya sasa ni 50 kwa 50 kutokana na ukweli kuwa WANAWAKE nao hawakubaki nyuma kuzitetea haki zao, Lakini Kuna wanaume katika hali isiyo ya kawaida wameipokea ki vingine hiyo 50 kwa 50 na sasa wamekuwa wategemezi kwa wake zao na kujikuta wanakuwa wanyonge kwa wake zao! Mwanamke alipoitafuta 50 kwa 50 maana halisi ilikuwa kupunguza mfumo dume kama sio kuumaliza akilini mwa wanaume wengi, Majukumu ya familia ni yetu sote lakini ikifika mahala mwanaume akategea na kumuacha mwanamke akivuka 50 na kufika 70 ujue mwanaume anabaki na 30% kitu ambacho kinauvua uanaume wake na kumpeleka katika kundi baya wenyewe wanasema JAMAA KAOLEWA... Heshima ya mwanaume ni kuitwa BABA na ukiitwa baba iwe baba ya kichwa cha nyumba zaidi ya hapo EPUKA KUWA BABA MLEZI NI AIBU KWA MWANAUME.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz