MAMBO MACHACHE YANAYOTOA USHAHIDI WA MWANAUME AZINIYE NA MWANAMKE HANA AKILI KABISA. - EDUSPORTSTZ

Latest

MAMBO MACHACHE YANAYOTOA USHAHIDI WA MWANAUME AZINIYE NA MWANAMKE HANA AKILI KABISA.


1.Mtu pekee ambaye biblia imeagiza alindwe na mwanamke hata kama ni mtu mzima ukiacha mtoto, ni MWANAUME.
Kwanini? Ni kwasababu usipomlinda akianza kuzini nje ya ndoa, hutampata maana akili yake huibiwa kirahisi bila hata limbwata unaweza kudhani kalogwa.
Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume. Yeremia 31:22
Yaani hata lini utatangatanga ee mwanamke ukitaka kuiacha ndoa yako eti mumeo ni mzinzi ana mahawala kibao, hivi umesahau kwamba unaishi na mtu asiye na akili aliyetekwa ufahamu? Unahitaji kumlinda si kwa kumchunga kama mbuzi hutaweza, isipokuwa kwa maombi tu. Unataka kumwacha mumeo uende wapi? Msaidie usimkatie tamaa.
3. Ukitaka kuamini kama aziniye hana akili angalia yuko tayari kumpeleka QT hawala huku mkewe darasa la saba.
4. YUKO TAYARI KUONA FAMILIA IKILALA NJAA LKN SIO AZINIYE NAYE.
5. Ni rahisi kwake kushawishiwa na hawala akamfukuze mkewe, lkn hawezi kumsikiliza mkewe akimwamshauri aachane na mahawala. Hii ni ajabu na aibu kwa wanaume.
6. Yuko tayari kumnunulia gari hawala Huku mkewe hata kujifunza kuendesha gari anambania.
7. Anayeweza kuzini na mwanamke hata kwa macho na moyoni akamvua na nguo kabisa na kumaliza kila kitu lkn ni kwa hisia tu....hiyo mbinu anayeweza kuitumia ni mwanaume na mchawi tu.
8. Ni afadhari mtu aliyelogwa kutokuwa na nguvu za kiume kuliko mwanaume mzinzi na mwasherati asiye na akiri.
9. Ni afadhari aliyenaswa na mtego wa sigara isiyoongea kuliko mtego wa zinaa kwa mwanamke mwenye akiri.
~ Inaonekana hata limbwata inapenya kirahisi kwa mwanaume baada ya uzinzi kufanyika na kuondolewa akili.
10. Nionyeshe mwanamke mwenye akili aliyepewa mimba na kichaa mwokota makopo, Mimi nitakuonyesha mwanamke kichaa aliyepewa mimba na mwanaume.
11.Ni afadhari kumshauri mlevi wa mvinyo baada ya ulevi kumtoka kuliko mlevi wa zinaa, maana ulevi wake unaendelea kumtafuna hata akiwa peke yake.
Bahati mbaya ni kwamba uzinzi unakaa kwenye ufahamu wa mwanaume kama doa lisilofutika na huenda kusumbua watoto wake na ujukuu pia .....unakuta wanasema yaani alivyo huyu kijana babaye au babu yake alikuwa malaya hivyo hivyo.
Mithali 6:27-29,32-33
Je! Mtu aweza kuuzima moto kifuani pake, na nguo zake zisiteketezwe?
Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, na nyayo zake zisiungue?
Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.
Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;
Wala fedheha yake haitafutika.
USHAURI
Ukiwa mwanamke ameokoka na una mwanaume asiye na akili ombea sana nafsi yake inasulike ilikonasa wewe una nafasi kubwa sana ya kumbadirisha maana uko mwili mmoja naye japo amefanya maagano na miili mingi ya nje.
Na kama nawewe hujaokoka okoka basi ili ndoa yako irudishwe paradise usilipize kisasi ukaanza kutoka nje wakati una akili zako timamu! Siku hizi magonjws ni mengi.....Epuka kumoigia kelele hizo hazisaidii wala hazijawahi kumgeuza, wala usipigie siku hawala zake utaumia bure.
~Acha kupeleka kesi zako za uzinzi wa mumeo kwa wazazi wako wala wake haitakusaidia ile siyo akili yake.....ipeleke ndoa yako msalabani pa mwokozi anayerejesha akiri na nafsi ya mtu iliyonaswa.
ZAIDI YA YOTE ANA HERI MWANAUME MWENYE HOFU YA MUNGU NA KUMPENDA MKEWE NA KUJARI FAMILIA YAKE.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz