KWANINI UCHUMBA NI DARAJA LA NDOA? - EDUSPORTSTZ

Latest

KWANINI UCHUMBA NI DARAJA LA NDOA?

Image may contain: 2 people, people smiling, ocean
Kwanza kabisa ijue maana ya DARAJA! Daraja ni kiunganishi cha barabara lililotenganishwa na MAJI... Kwa namna yoyote ile uchumba ndiko sehemu ambayo WANA NDOA watafahamiana na kuzijua tabia zao za siri, Ndoa nyingi ama mahusiano mengi yamekosa mvuto kwa sababu ya urahisi wa muingiliano wa ki mwili, Yaani watu wanatongozana leo na siku hiyo hiyo wanaanza maombi ya kuoana, Rafiki hata kazi ya House Boy au House Girl mwajiri hupenda kujridhisha tabia za mtumishi wake hata kabla hajakubari amfanyie kazi ndo maana kuna swali kwa wenye CV zao "UDHOEFU" Sasa hata mimi natamani kama mtu anapokuwa anamtaka mwenzie "MWANAMKE" aulizwe ukomavu wa akili na uvumilivu wa skate za wadada ameupatia wapiiii? Kwani wanaume wengi wanampenda Mwanamke akiwa amevaa na ukiisha mvulia nguo anatimiza adhima yake na kusepaaa... Dhamana ya PENDO IKO NDANI YA MOYO WA MWENYE UPENDO na ukitaka kuamini kila mwenye UPENDO WA DHATI huathirika sana pindi anapogundua amefanyiwa usaliti na Mtu aliyempa moyo wake, Wasokuwa na UPENDO hawajui kuumia maana hana mtu mmoja kichwani mwake, hivyo ni ngumu sana Kuumizwa na mtu mmoja laa wote wamuache ama kumuumiza... Usimpe mtu MOYO wako kabla hujajua kama anao upendo wa kudumu, Wapo wenye kumpenda mtu kwa sababu ama nyakati na baadaye hukinai na kuondoka, Sio kila mwenye maneno matamu ndani yake ni Mtu, Wako wanaongea maneno matamu lakini mioyo yao imeficha tabia za SIMBA/CHUI hawakawii kukuralua, JIPIME KI FIKRA KABLA YA KUMPENDA MTU maana ukiisha jikita kwenye UPENDO juu ya Mtu na akawa sio wa fungu lako UTAISHI KWA MATESO maana tayari uliisha jifunga kwenye NDOA.
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria 🙄
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz