Kinachotesa MAHUSIANO/NDOA nyingi ni WAWILI HAO KUSHINDWA KUUVAA UHUSIKA WAO! - EDUSPORTSTZ

Latest

Kinachotesa MAHUSIANO/NDOA nyingi ni WAWILI HAO KUSHINDWA KUUVAA UHUSIKA WAO!

Image may contain: 1 person, sitting
Watu wanaingia kwenye MAHUSIANO/NDOA kwa speed ya ajabu lakini baadaye akibaini hayuko sehemu salama anakata tamaa na kujutia lakini tayari anajikuta AMENASA pengine kwa muonekano wa Mtu na akashindwa kuchomoka, WAPENZI wameshindwa kabisa kujua maana ya MAHUSIANO na badala yake wamejikita kwenye kutoana JASHO JEMBAMBA na wengine kutumiana kwa masrahi binafsi... WANANDOA nao usiombe hao ndo wako kwenye hatari, Kila mmoja na yake MICHEPUKO🤣
Ndoa zinalindwa na;
JAMII ITANIONAJE?
DINI ITANIONAJE?
Kwamba watu wangu walioshiriki kunichangia na ndugu kushiriki harusi je wataelewa kwamba NILIKOSEA KUOLEWA/KUOA MTU HUYU?
Nitaingiaje msikitini/kanisani na nimevunja ndoa ambayo waumini wenzangu walishiriki na wao hawajui mateso napitia kukosea kuolewa ama kumuoa huyu mtu?
Mwisho wa siku kila mmoja na chumba chake ili kujinafasi huku jamii ikiona watu hao ni MUME NA MKE!
Na hapo ndipo kila mmoja ataanza kujitengenezea UHURU wake ili kuitafuta AMANI YA MOYO... Mahusiano/ndoa za sasa zimekuwa kama KARANGA kwamba haimalizi njaa ila unaweza kusogeza muda wa kula🤣🤣
Lakini Kuna wakati KARANGA inaweza kukusababishia kiu cha maji ukiweka lita moja tumboni UMESHIBA💃
Ndo maana MAHUSIANO/NDOA nyingi za kizazi hiki wengi wameji-TUNE kuliko kuvunja ndoa jamii au dini ikahoji KILA MMOJA AWE NA WAKE PEMBENI tukirudi home tunagawana majukumu kitu ambacho ni HATARI SANA! MOYO wa mtu ni giza je unajua Mwenzio anakuwazia yapi? Kwa sababu mnaweza kuishi kwa kulinda KANISA/MSIKITI mlio fungia ndoa JE MNAWEZA KUILINDA MIOYO YENU ISIUMIE?
Mungu hapendi KUACHANA isipokuwa UZINZI TU... Ninyi mshakuwa wazinzi MUNGU AMEKUBARI MUACHANE IKIWA MTU AMEZINI NJE YA NDOA! Unangojea hukumu ya MKEO/MUMEO kwa wivu anaosikia juu yako?
Pamoja na kukusaliti pengine analo pepo tu ila ANAKUPENDA na kingine kinachoumiza ni MUDA pale mtu anapoangalia madharau yako na aliwekeza muda wake wa miaka kadhaa leo unamuona hafai JE UNAJUA ANAKUTUNGIA SHERIA GANI? Msaada kwenye NDOA/MAHUSIANO yenye migogoro ni;
KUMALIZA TOFAUTI ZENU.
KUACHANA KILA MMOJA AKASEPA.
Vinginevyo unajitengenezea bomu ambalo wewe mwenyewe ndiye utakata uzi LIKULIPUKIE.
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria🙋🏻‍♂
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz