Jiulize swali hili; KWANINI MAHUSIANO YA SASA YAMEKUWA MARAHISI? - EDUSPORTSTZ

Latest

Jiulize swali hili; KWANINI MAHUSIANO YA SASA YAMEKUWA MARAHISI?

Image result for sanchiworld
Kwa upande wangu ninachojua ni kwamba;
"Ili mahusiano yawe imara na kujenga dhamana ya upendo ni wajibu wa walioyaingia kunia mamoja"
Kinyume chake labda kama walivutiana kulingana na haja za ki mwili ama urafiki wa kawaida, Unajua Kuna mahusiano ambayo watu wanaishi kwa KUHITAJIANA KWA WAKATI MAALUMU iwe ni kampani ya starehe au kipindi cha mhemko, Uhusiano huo nao Una watu wake na wala sipendi kuwaingilia, ninao weza kuusemea Mimi ni UHUSIANO ambao MTU ANAAMUA KUMHAKIKISHIA MWENZIWE KWAMBA ANAMPENDA NA ANAMHITAJI.
Kwa sasa;
MAHUSIANO YAMEKUWA RAHISI KWA SABABU MAANA YA MAHUSIANO WENGI WAMEJIKITA KWENYE NGONO ZAIDI KULIKO UPENDO.
Sio Mwanamke wala Mwanaume Yaani sasa hivi kabla ya mtu kujikita kwenye UPENDO anaanzia kwanza kwenye "KUDINYANA" akikolezwa ndo anajenga mazoea mwisho wa siku anajikuta kapenda, KUPENDA wewe haimaanishi na mwenzio ATAKUPENDA maana kama wewe ulitamani na baadaye ukapenda Una hakika gani kama nae ameridhia kukupenda?
Fumbo la MAHUSIANO linabaki kuteguliwa na wahusika, Kwa sababu UPENDO haujifichi na Una tabia ya KUNG'ANG'ANIA kwa maslahi mapana ya NAFSI.
Majibu ya swali langu kwamba;
KWANINI MAHUSIANO YA SASA YAMEKUWA MARAHISI ni kwamba huwezi kujinasibu uko kwenye MAHUSIANO wakati Mtu uliye nae hajui kama anakupenda, na sababu hiyo inatokana na ukweli kwamba TAMAA imetangulia badala ya UPENDO kwamba mtu anaingia kwenye MAHUSIANO kwa kujaribisha kwanza ili VIGEZO NA MASHARTI vikikidhi ndipo anajibwaga, Wakati huo huo upande wa pili hatujui kama nako umebadili mtazamo, Mwisho wa hayo MAHUSIANO YA SASA YATAENDELEA KUWA MARAHISI Kwani wengi tunaamini katika "KUDINYANA" kuliko uhalisia wa mahusiano ambao ni;
MAHUSIANO NI KUNIA MAMOJA kati ya wawili Yaani Mwanamke na Mwanaume ambao wameamua kujenga UMOJA wao ili KUTENGENEZA DHAMANA YA MIOYO YAO ili kuweka maslahi muhimu kama UPENDO, HESHIMA, pamoja na kufikishiana HISIA zao kinyume cha hayo huo ni UZI-NZI TU.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria 😎
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz