JE WINGI WA MISAMAHA NI SURUHISHO LA MAKOSA AMBAYO YANAUMIZA UPANDE WA PILI? - EDUSPORTSTZ

Latest

JE WINGI WA MISAMAHA NI SURUHISHO LA MAKOSA AMBAYO YANAUMIZA UPANDE WA PILI?

Image may contain: 2 people, people smiling, people sitting
Kwanza kabisa TABIA ni kama ngozi, Hata kama utapaka mkorogo wa aina gani rangi yako kwa uhalisia haitapotea sehemu yoteπŸ˜‚πŸ˜‚
Ki maandiko tunaagizwa kusameheana, Ki bin adam tunaagizwa kusameheana 7 × 70 lakini huyo anayepewa msamaha anatambuwa kwamba alimuumiza mwenzie? Naweza kusema kwamba MSAMAHA UNATAJWA KWA MAMBO AMBAYO UKIISHAMJUWA MTU UNAKUWA NA MAAMUZI YA KUENDELEA NA UKARIBU NAE AMA KUWA MBALI NAE... lakini unapozungumzia Swala linalogusa MAPENZI unakuwa umegusa nafsi ya mtu, Kuna watu HAWABADILIKI hata kama utamuonea huruma na kumsamehe 100 × 100,000 Still atakuwa ni yule yule na kwa matendo yale yale😭
Msamaha raha yake Mtu akiri kosa na kosa hilo lisijirudie, Ni rahisi kuendelea kumsamehe Mtu ambaye makosa yake hayajirudiii Kwani ndani yake mna UKOMAVUπŸ’ͺ🏽 siku moja udhaifu wake utakwisha na hawezi kukuumiza, Ila mtu anayeweza kukosea leo na kosa hilo likajirudia mara kwa mara ndani ya miezi 6 kuanzia leo UJUE HIYO NI TABIA YAKE AMA LAA NI KITU AMBACHO HAWEZI KUKIBADILI KITOKE KUWA KOSA KWAKUWA HAJUI KAMA ANAKUUMIZA NACHO! Kwenye MAPENZI hatupashwi kuumizana makosa ya kujirudia, Hatuwezi kukwepa kukoseane na kusameheana kwa makosa ambayo hayajirudiii ili tutimize maandiko yasemayo MAKOSA HAYANA BUDI KUJA ILI KUTUPA UKOMAVU ila sio kwa Mtu ambaye anaahidi kubadilika kwa kosa alilokukosea na akiishaona mko Sawa kosa lile lile linajirudiaπŸ˜‚
kwa mfano wa kosa;
UMEGUNDUA MWENZA WAKO ANAKUSALITI AMA KUNA MTU MWINGINE NAE ANAJUA YEYE NI WAKE WAKATI HUO HUO WEWE ULIAMINISHWA UKO PEKE YAKO, PENGINE UKATAKA KU-BREAKπŸ”Ί NDIPO MTU AKAOMBA MSAMAHA NA UKAKUBARI YAISHE... Baada ya muda unagundua bado yupo na huyo mtu BADO UNATAKA NIKUSHAURI KWAMBA UNADANGANYWA? Hapo huna chako zaidi unapotezewa muda mwisho wa siku ATAKUONDOKA UFE KWA BP🀦🏾‍♂
Muda mwingine MISAMAHA hujenga udhaifu upande wa pili, Yaani Mtu anapokuwa amejua udhaifu wako ni rahisi kukosea na akainuka kukubembeleza ili umsamehe, Kama anajua kosa lake hawezi kulirudia wala hataweza kuomba msamaha kwa kosa lile lile πŸ™‹πŸ»‍♂
Ukiona Mtu anapenda kukuomba misamaha ujue MAMBO mawili:
AMEKUZOEA
ANAKUDHARAU
Kwa mtu aliyekuzoea maana yake anajua atapambana nawe kwa njia gani ili umsamehe, Kwa Mtu anaekudharau atajishusha ili akurejeshe kwenye nomal na baadaye ataendelea na tabia yake, Uwe mkali mtu anaporudia kosa na ukiona hakuna mabadiliko SOMA GAPE kama konda wa daladala🚌
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz